JAY THE SON
Member
- Nov 26, 2017
- 43
- 33
Nawasalimu ndugu zangu watanzania bila kujali itikadi za vyama vilivyopo nchini kwetu nikubali pia mie ni miongoni mwa watanzania wengi tunaokubaliana na dhana nzima ya mabadiliko yawe binafsi au nchi kwa ujumla na bila hiyana nikubaliane pia na mabadiliko hasa yanayoendelea kuonekana nchini kwetu pamoja na kuwa mabadiliko hayo yamejikita katika upande mmoja wa shilingi wakati upande wa pili ukiwa bado haujaliona jua
Niwakumbushe pia ya kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kauli mbiu na agenda kubwa karibu kwa vyama vyote shiriki katika uchaguzi huo ilikuwa ni mabadiliko baada ya kuwa tumeona madhaifu mengi sote tukakubaliana ni wakati wa mabadiliko bila kujali angeingia nani ikulu lakini dhamira yetu ilikuwa ni mabadliko hata kukawa na ishara nyingi ili kuipa agenda hiyo uzito wapo walio zungusha mikono ili kuonesha na kuipa nguvu dhana hiyo lakini pia upo upande uliomnadi mgombea kwa kusema fulani kwa mabadiliko bado tulibaki kukubaliana kuwa tunahitaji mabadiliko jambo ambalo lilijikita katika kuonesha dhana pana ya kiuchumi kisiasa na kijamii.
Swali ambalo mbali na mapungufu ninayoyaona ni nini haswa watanzania tulitaka kibadilike je ni uongozi wa chama x kwenda chama y au uendeshwaji nchi uliokuwepo kwa wakati ule
Ndugu zangu tukubali tukatae ktk kuyaendea na kuyafikia mabadiliko ni wazi upo upande ambao lazima utaumia na upo upande utakuwa mfariji kwa ule unaoumia kiongozi mkuu wa nchi hawezi kufanya mambo ambayo yatamfurahisha kila mmoja na katika kupingwa ndio changamoto ambazo humpelekea kiongozi kufikia lengo lake mendeleo yanahitaji kujifunga mikanda na sote kwa kauli moja nchi itaendelea nikiri wazi wapo baadhi ya viongozi wanaoamini na wanaendelea kuamini ili uendelee ni lazima usiwe na mpinzani dhana ambayo imepitwa na wakati ili ushinde mbio lazima awepo anayekukimbiza na hata ukishinda hupaswi kujisifu pekee kuwa unambio wapaswa kumsifu na anayekukimbiza na baadhi ya hawa viongozi hutaka kutuaminisha kuwa maendeleo ya kweli hsyafikiwi kwa sababu ya uwepo wa upinzani kitu ambacho sio kweli maendeleo yoyote yansletwa kwa kodi za wananchi na nchi husika na sio kwa sababu eti kuna upinzani .
Tanzania ni yetu tunapaswa kuilinda kuitunza na kuithamini itikadi za vyama visitugawe sote tuko na dhamira moja ya maendeleo na mabadiliko mwisho niseme tena maendeleo na demokrasia ni vitu vinavyoshabihiana huwezi kufanya maendeleo wakati huo huo unaminya demokrasia ili maendeleo ya kweli yawepo lazima tufungue milango ya kukosolewa lengo likiwa ni sote kufika tunapopataka tumemuamini nahodha tumuache atufikishe bandarini salama tutapigwa na kila aina ya dhoruba lakini bandarini tutafika salama