mojax
Member
- Aug 18, 2015
- 13
- 23
ELIMU BIASHARA
MABADILIKO NI WEWE
Sikuzote tusiamini kwamba maisha yetu yatakuja kubadilishwa na mtu, la hasha, Maisha yetu yatabadilishwa na sisi wenyewe, Mabadiliko yanaanzia ndani yako mwenyewe na nafsi yako. Mtu wa nje anaweza akakushauri tu au kukuonyesha njia nzuri ya kubadilika. Na kuna wakati kuna watu tunakaa tunasubiri mtu aje kutukomboa, tunasahau kwamba huyo mkombozi ndio sisi sisi ambao watu wa zamani nao pia walikua wanamsubiria.
Ila sisi tumefumba macho tukiamini kwamba labda bado kuna mwingine tuendelee kusubiri. Kuna watu tuna imani sana na wanasiasa kwamba wakiingia wao kila kitu kitabadilika. Juzi nimekuta mtu ukuta wa uwani wa nyumba yake umebomoka upande mmoja, ila amekodi Muziki ameweka kigodoro kwake watu wanacheza na kunywa, je Haikua ni busara kutumia gharama zile kukarabati nyumba yake kwanza? Mwanasiasa anaweza akaja akawatia uongo, alafu akawaambia Mkimchagua atawatengenezea Barabara toka Mkulanga kuelekea Mbinguni na Mkapata shortcut ya safari ya kwenda Mbinguni, na Mkachanga, si Hamnazo.
Maisha yetu hayatabadilishwa na mwanasiasa, hata kama mwanasiasa akisema kodi ishuke iwe asilimia 2% kama ulikua haufanyi kitu kinachokuingizia kipato ambacho kodi ilikua kikwazo huwezi kuona umuhimu wala faida yake. Hata kama akisema mikopo Bank ishuke riba iwe asilimia 10%, kama hauna biashara ya kukuwezesha kukopa ukuze mtaji bado hutaona kama ana faida kwako, swali la kwanza ni wewe unafanya nin? Kabla ya kujiulize mwanasiasa atakufanyia nini. Kumpenda Mwanasiasa hakukufanyi uwe na Maisha Mazuri, sawa na Kumpenda mwalimu wa Hesabu hakukufanyi ufaulu Hisabati.
By Man Dea
Instagram: Elimu_biashara

Last edited by a moderator: