Hassan Longoi
New Member
- Apr 28, 2015
- 3
- 7
Wasalamu wana jamvi
Ndg wanajamvi wenzangu tumekuwa tukijadili mambo mengi katika jamvi hili ya kisiasa,kiuchumi na kijamii. Yote hayo ni ktk kulijenga taifa letu. Taifa lolote duniani hujengwa na raia wake, nami ni raia mwenye wajibu kama huo.
Ili Taifa liendelee na Kustawi vizuri tunahitaji kiongozi (viongozi) imara wenye kuafikiana na watu wao (bila vitisho) na wawe na maono ya kuleta maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo ama ujuzi/maarifa toka nje yenye nia nzuri ya kuleta maendeleo kwa watu wake (Govt to be accountable for the people) sio wananchi wahudumie serikali kama ilivyo sasa (mf. michango isiyoisha-lramba ijulikanayo kama Malalo) ambapo wananchi hulala na kuamkia kwenye janga la michango bila kushirikishwa!! Yaani hapa viongozi wanapanga mipango ya maendeleo (bila kuwashirikisha) wananchi wanapokea mipango wasioijua mwisho wake!! Viongoz hufikiri kwa niaba ya wananchi, na kujifanya wajuzi kujua na kuweka mipango ya maendeleo ya wananchi kuliko wananchi wenyewe wanaowatumikia. Wananchi hudhaniwa hawajui chochote.
Elimu ikiwa chini ya kiwango, michango lukuki, lakini bado viti vya wanafunzi ni visiki, mawe au tofali loo!! Shule zinaendeshwa kwa michango ya wananchi mfano mitihani ya ndani mashuleni (January-Desemba) michango ya kulipa walimu wa elimu ya awali, maabara, walinzi, madawati nk.
Yote haya wananchi hufikiriwa hawawezi kusema chochote mpaka wasubiri sera ya chama fulani (ilani) ili waje kupangiwa cha kusema na kufanya!!! Suala la maendeleo ni mzunguko kama mitala.
Matatizo ni mengi sana, Siasa za jimbo la Iramba Magharibi ni za kizamani -vitisho na kubambikiziana kesi.
Umefika muda wa kuwapatia wananchi siasa safi (uhuru wa kuchagua viongozi)......orodha ni ndefu ya mambo ya kubadilisha.
Kwa kero hizi nilizozitaja na ambazo sikuzitaja hazivumiliki.
Kwa ujasiri mkuu (paramount voice) Mimi Hassani Longoi Natangaza nia kugombea UBUNGE jimbo la Iramba Magharibi (SINGIDA), kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ridhaa ya wanachama ni muhimu, Ridhaa ya wanairamba ni muhimu zaidi, Maendeleo kwa wana-Iramba ni lazima chini ya Kiongozi mwenye maono ya maendeleo kwa watu wake sio wale wanaojifanya watoa misaada (fedha zake mfukoni) wakati hali halisi ni kodi za wananchi (mfuko wa jimbo). Jimbo si kambi ya wakimbizi pa kujikweza kutoa misaada badala ya kuweka misingi kwa wananchi kujikomboa kiuchumi.
Dira/Vision & Mission
1. Kufuta michango yote inayo waumiza wanachi wengi wenye kipato kidogo.
2.Utawala shirikishi-wananchi ndiyo wapanga maendeleo kwenye maeneo yao (people's power)
3. Kusimamia mapato ya jimbo (kodi) kutumika kwa manufaa ya wananchi na sio posho za vikao
4. Kurejesha siasa za ushindani za vyama vya siasa (civilized politics) bila kupandikiza chuki (Movement for Peace- M4P)
MAONI YANGU KUHUSU UPATIKANAJI VIONGOZI (Wabunge, Madiwani na Rais - 2015)
Tuwe na mijadala ya wazi (mahojiano ya hadhara -public interview) Mfano, Wabunge wenye dhamana ya kutunga sheria za nchi, ni vyema watanzania waanze kuzifahamu dhamira zao kwa taifa kupitia midahalo ya hadhara. Hii itasaidia vyama vyote kupata wagombea sahihi sio watakaowazidi wenzao kwa kugawa sahani za wali na viroba vya pombe.
The first responsibility of a leader is to define REALITY.
The last is to say THANK YOU. In between, the leader is
a SERVANT!
HASSANI LONGOI