Mabadiliko kwenye sera ya elimu...

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Hamjambo waungwana ...
Kila siku kilio ni kile kile kuhusu elimu kufanyiwa mabadiliko kisera. Kwa maoni yangu ni kwamba hayo mabadiliko tayari yalishafanyika ila wananchi ndo hawajajua.

a) Hakuna kiongozi wa nchi ambaye mtoto wake anasoma shule za serikali - ni kwa sababu wanajua kuwa kuna mabadiliko.

b) Hakuna mtoto wa mwenye nazo anayesoma kwenye shule za serikali kwa sababu tayari kaambiwa kuwa kuna mabadiliko.

Tunachokiona ni mpango mzima wa kuhakikisha wanazalishwa wananchi ambao uelewa wao ni kuendelea kuwaheshimu hao watunga sera. Serikali sio Jitu wala Chombo, ni kikundi cha watu wanaopanga namna ya kuendelea kutawala sehemu fulani - ndo hao hao wanaojua kuwa elimu ya Tanzania ni mbovu na hivyo watoto wao hawawezi kuwapa elimu hiyo.

Taasisi zinazofanya kazi ya ku-regulate elimu zinahakikisha zina-regulate hadi iwe hovyo kabisa. Hazifanyi maboresho na badala yake zinaharibu kabisa.

1. Hivi inakuwaje unampeleka mtu alionesha uelewa mdogo kwenye masomo ndo aende kufundisha wenzake?

2. Inakuwaje mtu asiyejua hesabu aende kusomea ufamasia?

3. Mtu aliyeweza kutengeneza siraha - iweje umfunge badala ya kumuendeleza kwa ulinzi maalumu?

4. Wapo watu waliokuwa wabunifu na waligundua vitu vingi lakini serikali hii hii ilihakikisha hawaendelei na jitihada zao za ugunduzi

Yako madudu mengi ambayo wote tunayajua - hayo yanawafanya vijana wetu wasiwe na moyo wa ubunifu, ukibuni kitu unakutana na vipingamizi. Kuna tafiti nyingi zimefanywa ambazo ukijaribu kuzifanyia kazi unakutana na taasisi ya serikali eti unaiingilia kwenye kazi zake.

Mfano: Jaribu kuzalisha umeme kwa njia utakayoweza, upange bei; upate wateja wa hapo unapoishi uanze kuwauzia ... utasikia eti umeingilia kazi za TANESCO. Hilo ni kosa kubwa na kuhujumu uchumi.

Nini kifanyike? Toa maoni yako!
 
nanukuu
"Hivi inakuwaje unampeleka mtu alionesha uelewa mdogo kwenye masomo ndo aende kufundisha wenzake?"

swali

kwahiyo serilkali iwafanyie redundancy watumishi(hasa waalimu) wa aina hiyo?

unadhani tatizo litakuwa limetatuliwa?
 
Hii nchi haiwezi kwenda sawa mpaka wale ambao hawataki kwenda sawa wakubali kupelekwa sawa la sivyo tutaendelea kua vibaraka wa watu wazito tu,kama ukipanda kibovu kwanini utegemee kuvuna kizima acha tuendelee kupata vibovu mpaka pale tutakapo kataa kua wapambe ingali tunajua upambe ni nuksi
 
nanukuu
"Hivi inakuwaje unampeleka mtu alionesha uelewa mdogo kwenye masomo ndo aende kufundisha wenzake?"

swali

kwahiyo serilkali iwafanyie redundancy watumishi(hasa waalimu) wa aina hiyo?

unadhani tatizo litakuwa limetatuliwa?
Wewe ni mwalimu au?

Ok! Nimeuliza nini kifanyike ... nawewe unaniuliza mimi tena? Ebu tuangalie maoni ya wengine!
 
Tufanye nini na lini?
 
Wewe ni mwalimu au?

Ok! Nimeuliza nini kifanyike ... nawewe unaniuliza mimi tena? Ebu tuangalie maoni ya wengine!
swali lako linainekana kuwa na solution ndani yake ndio maana nimenukuu hicho kijisehemu tu

ongea yote uliyotaka kusema juu ya hilo swali . kwa maana kwamba huwez kujiuliza tu bila kuwa tayari umesha pata majibu fulani ila tu umataka usikie wengine watasemaje.. funguka mkufunzi
 
Itakuwa vyema ukatoa jibu lako kwa yale uliyoyaona hapo kwenye uzi mkuu. Pili mimi sio mkufunzi wala sio mwalimu, mimi ni mkulima mwanaharakati tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…