Zapa RadioFm
Senior Member
- Feb 12, 2016
- 112
- 171
Maazimio ya Baraza la madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam lililoketi 02 mei, 2016.
1 . Taarifa ya viwanja vikivyopimwa na h/mashauri:Baraza limeagiza kupitia tena viwanja vya Kigamboni na mbia, kisha iandaliwe taarifa nyingine na iwasilishwe ktk kamati ya Mipango na mazingira na usafirishaji.
2:Mikopo kwa akina mama na vijana.
Uwekewe utaratibu na mfumo wa wazi katika kupata vikundi na DCB bank itatoa mikopo hiyo.
3:Ujenzi wa vituo vya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.
Baraza limeamua kuendelea kutumia kituo cha Ubungo wakati wakiangalia namna ya kujenga vituo vya Mbezi Luis na Boko basihaya.
4: Dampo la Mtoni lililofungwa.
Baraza limetaka kujua umiliki halali kwa sasa wa eneo hilo lililokuwa dampo kwa kuagiza wajumbe watatu kufuatilia, wajumbe hao ni mh Chaurembo, Mh Kafana na Mkuu wa idara ya Mipango miji, uzoaji taka na usafirishaji.
5:Taarifa kuhusu miradi ya Halmashauri ya jiji.
Baraza liliazimia kutembelea na kuijua miradi na mali za jiji na tayari ukaguzi huo umeanza.
6:Kuhusu vyanzo vya mapato ya Halmashauri.
Baraza limeagiza katika kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe ya kikao husika, mkurugenzi awakilishe taarifa kwa mstahiki meya wa Jiji orodha ya benki zinazotakiwa kulipa
Aandike barua kuzijulisha benki kwamba ulipaji wa Ushuru wa huduma za jiji(City Service Levy) ni takwa la kisheria
Ingawa halmashauri ya jiji inapata taarifa za benki kutoka benki kuu, mkurugenzi aliagizwa kumwandikia kamishina wa TRA barua ya kuomba taarifa za mapato halisi ya benki zilipo Dar es salaam, ili kujiridhisha na kiwango kinachotolewa na benki hizo wakati zinapolipa Ushuru wa huduma ya jiji (City Service Levy)
Imetolewa leo 9 Mei, 2016
Na Katibu wa mstahiki meya wa Jiji