stubborn wa Njombe
Member
- Dec 8, 2016
- 79
- 170
Habari za wakati huu wakuu.
Kama heading yangu inavyojieleza hapo juu nimekuwa na hayo maumivu sasa karibu mwezi. Nilishaenda hospital ya rufaa ya temeke kupima kwa kipimo cha ultra sound ila hawakuona tatizo lolote kwani walisema figo zote ziko sawa,ini ipo sawa kibofu cha mkojo pia hakina tatizo.
Kuna dawa walinipa za kutumia for 10 days nikimaliza nirudi tena niliporudi kwa sababu sikuwa na mambadiliko yoyote wakanibadilishia dawa. Nazo nikameza zilipoisha sikuwa na nafuu ikabidi niende hospital binafsi huko wakaniambia nina U.T.I nikachoma sindano za tano za power cafe.
Likazuka lingine la kupata maumivu ya kichwa na kuchemka mwili hasa ikifika mida ya saa sita za mchana. Baada ya kumaliza zile sindano ikabidi niende tena hospital safari hii walinipima typhoid na Malaria na U.T.I na vyote walinikuta navyo tena so wakaniandika dawa ambayo inamchanganyiko wa kutibu typhoid na U.T.I ila jina la hiyo siikumbuki vizuri.
Sasa dawa nimemaliza naona hali bado haijakaa sawa maumivu ya kwenye mbavu yapo vile vile na hizi homa nazo ikifika ile mida tu nakuwa mahututi ila haya maumivu ya mbavu nipiga myao ( yawning ) ndio yauma zaidi.
Naombeni msaada wenu wakuu hospital ipi inaweza ikawa msaada mzuri zaidi au ni dawa ipi naweza nikatumia ili niwe sawa kwa sasa hivi nimehamishia makazi yangu jijini Dar es salaam nipo maeneo ya Mbagala Zakhem