[Pia haijajibu matakwa na malalamiko
ya wananchi kwenye masuala
mbalimbali kama muundo wa Serikali,
miiko na maadili ya viongozi wa
umma, haki za binadamu, madaraka ya
rais na uwiano wa mihimili ya dola]
Mimi nilishasema suala sio watu kuisoma na kuona vilivyomo bali kuona ambavyo HAVIMO; hapo ndipo vilaza wetu wapinzani walipozidiwa akili na maaskofu hadi najiuliza kama nchi hii kweli kuna upinzani. Kazi kelele tuuu pointi hakuna.
Pia haijajibu matakwa na malalamiko ya wananchi kwenye masuala mbalimbali kama muundo wa Serikali, miiko na maadili ya viongozi wa umma, haki za binadamu, madaraka ya rais na uwiano wa mihimili ya dola.
...
Kimsingi hayo mambo hayo ndio moyo wa Katiba; ndio Katiba yenyewe la ajabu Katiba ya Chenge haisemi chochote tofauti na ile Rasimu ya Warioba. Tunarudi pale pale, kinachogomba sicho kilichomo (50/50, haki za wafugaji, wakulima, wavuvi, warina asali, n.k.) bali ambacho hakimo kama ilivyoainishwa kwenye red.