Waandamanaji mjini Hong Kong wamesababisha kuvurugika kwa mtandao wa usafiri mjini humo kwa siku ya pili mfululizo leo wakati mataifa ya magharibi yameeleza wasi wasi wao kuhusiana na machafuko yanayoongezeka baada ya polisi kumpiga risasi kijana muandamanaji na mtu mwingine kuchomwa moto.
Ongezeko hilo la ghasia ni la hivi karibuni katika wiki 24 za machafuko ya mfululizo yanayoongezeka katika maandamano mjini Hong Kong, yenye lengo la kupata uhuru zaidi wa kidemokrasi kutoka China.
Vikundi vidogo vya waandamanaji waliojifunika nyuso zao vilifunga barabara na kutupa vitu katika reli na kuzuia treni za mjini za chini ya ardhi na kusababisha mapambano na polisi wa kutuliza ghasia siku nzima.
Maeneo ya vyuo vikuu yamekuwa sehemu muhimu ya ghasia hizo ambapo Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji ambapo nao walifunga njia zinazoelekea katika chuo kikuu cha Hong Kong.
Taiwan Trump anaipa kichwa, anaiuzia silaha za mabilioni ya $s$ huku Hong Kong Ikipewa kichwa na UK ila kichapo heavy kikianza US/UK hawata onekana zaidi ya kukimbilia UN kuweka vikwazo.
Taiwan Trump anaipa kichwa,anaiuzia silaha za mabilioni ya $s$ huku Hong Kong Ikipewa kichwa na UK,ila kichapo geavy kikianza Us/Uk hawata onekana zaidi ya kukimbilia UN kuweka vikwazo.
Sifurahii Yanayoendelea Ila Kwa Umuhimu wa Kimkakati wa HONGKONG Kwa CHINA CHINA Wanaona Bora Wafe Waandamanaji Hata Wote Kama Ikibidi Ili HONGKONG Iwe Salama Na Mikononi Mwa BEIJING