Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
UKAWA na wanachama na wapenzi wake watii amri hii endapo CCM wanaitii. Wagombea wawakute watu kwenye eneo la tukio au watu wawakute wagombea pale; na wakati wa kuondoka wagombea baada ya mkutano wa kampeni basi wagombea waondoke kwanza then wananchi.
Nasema hivi ili kuonyesha amri hiyo si kitu chochote.
Na wakati wa kuondoka msubiriano ili isionekane mnaandamana mnaondoka kumi kumi kwanza.
Kwani maandamano maana yake ni nini? Iwe kama kwenye ibda ya misa kanisani kama wewe unajua taratibu za kanisani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Mecky Sadik amepíga marufuku maandamano ndani ya Dar es Salaam katika kipindi cha kampeni. Marufuku hiyo imepokewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamanda Suleiman Kova.
Kamanda Kova ametamba kuwa wanao askari wa kutosha na wenye nguvu na ari kwakuwa ndiyo kwanza wametoka Depo. Amewaonya wananchi wasitende kinyume cha Sheria na kusababisha kukamatwa.
Chanzo: ITV Habari