kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Demokrasia ina gharama zake, kuzuia maandamano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ni sawa na kusema kuwa kuwe na mvua za masika lakini kusiwe na mbu hata mmoja.
Shuhuli za kila siku za wananchi ni lazima ziingiliane na shughuli za kidemokrasia wakati wa uchaguzi kama vile kujiandikisha kupiga kura, uhakiki wa majina, mikutano ya kampeni, na zoezi la kupiga kura. Hata misafara ya Rais inakopita huwa inasababisha pia shuhuli za kawaida za wananchi kuathirika, na hiyo ndiyo gharama ya demokrasia tuliyoichagua sisi wenyewe.
Polisi wetu wanapozuia maandamano ya vyama vya siasa sio sawa, kwasababu huu ndio msimu wenyenye wa wananchi kukusanyika kwa shuhuli za kidemokrasia. Kazi ya polisi wetu katika kipindi hiki ingekuwa kutoa maelekezo na kusimamia namna mikusanyiko hii mikubwa ya wananchi itakavyopaswa kuwa salama lakini sio kujali malalamiko ya watu wanaoingiliwa shughuli zao za maisha kwasababu ya mikusanyiko ya vyama katika kipindi hiki kifupi maalum cha uchaguzi mkuu wa kila baada ya miaka 5. Hata bila ya maandamano haya ya wafuasi wa vyama vya siasa wako watu ambao wamewahi kuchelewa usafari, matibabu, kazini, sokoni, n.k kwasababu ya kuzuiwa na misafara ya viongozi wakuu wa kisiasa inapopita na migomo ya wafanyakazi, madereva au wafanyabiashara, lakini sijawahi kusikia polisi wakisema kuanzia leo misafara mirefu ya viongozi, migomo ya wafanyakazi, wanafunzi, madereva, wafanyabiashara au maandamano kwenye makongamano mbalimbali marufuku kwakuwa vyote hivi huwa vinaingilia shuhuli za wananchi wa kawaida. Hii ndio gharama ya demokrasia bana.
Polisi inapowazuia watu wasikusanyike kwa namna wanayotaka wao inasababisha watu wajiulize maswali mengi kama vile "ni kwa manufaa ya nani?" kwababu wanaoandamana ni wananchi na kazi zinazovurugwa ni za wananchi haohao, na muda, siku, eneo na sababu za kuvurugika zinafahamika pia, sasa ni nani wamelalamika? wapi? na wako wangapi?. hata kama watu hao wapo jibu lao lingekuwa kuvumilia kipindi hiki kifupi cha uchaguzi kiishe na kazi zao zitarejea kama kawaida baada ya uchaguzi kupita, sio kuwaridhisha kwa kuzuia maandamano kama "polisi" wanavyotaka ieleweke kwa wananchi.
Kipindi kama hiki ni kipindi ambacho kinavuruga shuhuli za wananchi duniani kote, hivyo haiwezi kuwa tofauti hapa Tanzania. Duniani kote hiki ni kile kipindi ambacho likizo zote za askari zinasitishwa na askari wastaafu wote wanarudishwa kazini ili kulinda usalama wa watu na mali zao katika misafara na mikusanyiko ya watu, lakini sio kuzuia maandamano kama walivyotangaza jeshi la polisi.
Mwisho wa ubaya ni aibu. Watanzania wote tunaongea kitu kilekile "maisha bora kwa kila mtanzania" lakini kwa lugha tofauti. Wewe kuwa polisi haipaswi kukufanya usione uchungu wizi wa pesa kama zile za escrow ambazo zingeweza kusogeza maisha ya shangazi yako kule kijijini kama zingewekezwa kwenye upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati zetu vijijini, hupaswi kusahau kuwa ukistaafu nawe utakwenda kuishi maisha ya kawaida sehemu isiyokuwa na maji ya kufulia. Yatupasa sisi sote tuchanganye na akili zetu kwa kila jambo.