Je watu wakiamua kuandamana wote na kulala barabarani kuanzia posta mpaka kimara, mpaka mbezi beach, watapitisha wapi hayo magari ya maji kuwasha na ya mabomu au watatumia ndege? je wanayo hiyo ndege? Saa nyingine watawala wafikirie sana maana iko siku watu wata data wenyewe! yakumbukwa mapinduzi ya zanzibar wala hayakuwa na maandamano na haykuwa na upingamizi, jamaa wameamua tu kusema imetosha jamaa wakaanza! kila siku tunayasifu na yapo kwenye historia! je watu hawajui kwamba..."what goes around comes around?" inabidi watawala wetu waamke maana wa TZ ni wengi mno kuliko polisi na wanajeshi waliopo. Ni wengi pia kuliko hata risasi zilizopo na hata vifaru na vifaa vingine vy kivita havitauweza umma wa waTZ wakiamua kusema yatosha!!!! Ukiona mwenzio ananyolewa wewe weka maji. Tunisia, Misri, Yemen, hawajamtukana Mungu! Tuliombee Taifa letu tupite kwenye mageuzi kwa amani, tunahitaji mageuzi ya kiuchumi yenye kuleta tija kwa waTZ wote na sio kwa wachache! Uchumi wa nchi hii yamkini umeshikiliwa na karibu asilimia 10 ya wananchi na wengi wao, wanakoo zao huko nje ya TZ. Hii si kitu ya kujivunia hata kidogo!!!!