Maana ya utawala bora,
Ni usimamizi wa rasilimali za nchi kwa minajili ya kuwepo na uwazi,uwajibikaji,,usawa, nakujali mahitaji ya wananchi. Mwalimu Nyerere alisema bila ya utawala bora hatuwezi kupambana na umaskini. Na kinyume chake umekuwa utawala mbovu wenye sifa hizi; umejaa rushwa, matumizi mabaya ya mali ya umma, kutokuwajibika, ucheleweshaji wa mifumo ya serikali, urafiki au undugu katika kupata uongozi, serikali kutojali mahitaji ya wananchi wake na mgawanyo wa raslimali za nchi,ukwepaji kodi n.k.
Tumeshuhudia mengi yanayofanana na utawala mbovu kama kama ukwepaji kodi,wizi wa raslimali za nchi kwa kisingizio cha uwekezaji kama mikataba ya madini,gesi n.k Umasikini tulio nao watanzania chanzo chake ni serikali ya magamba(ccm),kilimo ndio nyenzo kuu ya kuondoa umaskini nchini iwapo wakulima watashirikishw katika sera za kilimo.
Lakini kwa bahati mbaya sana,serikali imekuwa ikija na sera/programu bila kuwashirikisha wadau,semina zenyewe zinafanyika kwenye mahoteli makubwa ambako hata hakuna mkulima. Wameleta sera ya kilimo kwanza na mapawa tiller kibao ambayo yamegeuka kubebea tofali nk.
Matokeo yake powertiller zimekuwa ni sehemu ya kuombea kura!! Hatuwezi kuondoa umaskini kama hakuna utawala bora,ushirikishwaji wa wakulima katika kuandaa sera n.k,miundo mbinu ya barabara na umeme.
Nawasilisha wadau!