aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 792
- 1,144
Unaweza kumjuwa JPM kwa urahisi sana anapolitaka lake. Kumtembelea maalim alipokuwa Serena baada ya kuumwa lengo ni kumpooza tu kwa Umakamo wa Rais baada ya kurudia uchaguzi ambao jamaa walishapanga tu washinde. Alisema kwamba “tunamhitaji apoe akafanye kazi”. Aliiona kazi rahisi sana kwa maslahi yake na chama chake. Waliuamoaminisha kuwa hili linawezekana wamemuweka njia panda na ndio maana kafura baada ya kukosekana alilolitaka.
Pili ni kwa Lipumba na ile ziara ya JPM baada ya kuapishwa. Kumbe alikuja kuleta ujumbe turejee uchaguzi, tukubali kushindwa na kuwaendea kinyume wananchi ili Umakamo uwepo. Hesabu zake Lipumba hapa nae lazima ufikiri aliahidiwa nini? Mkono mtupu haurambwi nae kagonga mwamba, hakuwa anaeaminika tena.
Lilipo ni kuwa watawala watakubali uchaguzi urejewe baada ya Lipumba kuzivamia ofisi zetu na kushiriki na vibaraka wengine pamoja na fisi ili wagawiane Zanzibar kama ile heligoland treaty ya wajuramani. Polepole alisema miezi mitatu, naam kama mchezo wa karata na ujuha walionao. Wala si 2020 bali ni pale watapofanikiwa kwa Lipumba na genge lake kuzivamia ofisi halafu wakubaliane na CCM kuunda interim na uchaguzi mwengine wa CCM A na CCM B.
Mutungi nae ana maslahi yake kwa hapa, maana kabugi step kuzipoteza fedha za umma kinyemela. Hizi kesi zikithibiti kuwa hakulifanyia taifa haki na hadaa hii ya milioni 360 basi anajivua nguo na anaweza kabisa huko mbele akasimama mahakamani kwa ufisadi wa fedha za umma.
Halafu kuna mafisi wao haja yao ni third alternative Zanzibar kwa gharama yoyote ili mradi tu waambiwe nao wanajimbo wameshika. Hesabu zao kuwa hili litaiuwa CUF na tutaelekea kule kule nao kuwa sehemu ya mgawo wa ngawira ati kwa maslahi ya taifa, wanakwambia taifa kwanza.
Kuna mstari wa stahamala kwa yoyote anaesukumwa katika uonevu. Hisabu zao na kauli za CUF zinazosema wazi wazi mutalitia taifa katika makubwa kwa upuuzi wenu basi mulitafakari sana. Munapotaka kuwapeleka watu walioamini katika nguzo ya mabadiliko kwa miaka hamsini ni majuto makubwa siku za mbele. Mutabeba misalaba ya ujuha huu musioutambua.
Target si CUF bali umoja wa upinzani. Si unaona katika chama chake malaika kahakikisha hakuna mwengine wa kumpinga 2020? Tumebaki wapinzani na umoja wetu tu unaomshughulisha. Anajuwa kashinda vipi 2015 khofu tu ya malaika vitabuni. Akili zao kuwa Khalifa na Mnyaa watawasaidia ati kwa Pemba, wanasahau kura za pemba 2015 kwa CUF NI 99,000 tu, bado wamejawa na utoto wa kutoona mbele, tumeshinda 2015 kwa kukubalika kila mkoa visiwani.
Fikiri si walishiriki walioitwa wapinzani katika uchaguzi wa March? Wengine so wameunda mpaka sirikali ya umoja na kupewa nyadhidha za uwaziri? Jee hilo genge la Lipumba litafika wapi wenzao kina Hamadi Rashid walipokuwa hawapo? Jee umma umetetereka? Wanapowasukuma watu huko mbeleni watajutia maamuzi yasio kina cha utu. Wakti huu si ule.