Maalum kwa kina dada: Utajua vipi kama mwanaume hana mopango wa muda mrefu na wewe?

tethering

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
331
139
Hii ni taarifa maalum kwa kina dada. Je utafahamu vipi kama jamaa hana mpango wa kukufanya mpenzi wake au pengine hata kufunga ndoa na wewe siku moja? Utajua vipi kama jamaa anataka ngono tu na anakutumia kama kifaa cha kutimiza lengo lake hilo? Mtaalam wa mapenzi na mahusiano, Ethel DeGroodit wa Marekani anaweka wazi viashirio vitano, ambavyo ni lazima uzingatie, ili kumgundua mwanaume wa aina hiyo, ili kama lengo lako ni ndoa, basi ujue imekula kwako.

Mazungumzo yake ni mafupi mafupi: Mara nyingi wanaume wanaotaka ngono tu, huwa hawana mazungumzo marefu na mwanamke husika, kwani wanaogopa kuwa na mazungumzo marefu, ambayo yatapelekea wao kujichanganya, na pengine kusema kitu ambacho hawakukusudia kusema, au kwa maneno mengine wanataka kuficha. Mtaalam DeGroodit anasema. Kazi ni kwako wewe mwanadada kuchunguza na kufuatilia mazungumzo yao, ili kubaini kama kuna ujanja ujanja wowote.

Hapigi simu kwa lengo la kuzungumza tu: Kama hapigi simu na kusema “Hey mpenzi! Nilikuwa nakupigia kufahamu tu unaendelea vipi (nimekumiss)”, basi ujue kuna mtu anayepigiwa na kuambiwa maneno hayo, na mtu huyo si wewe. Kwa maana nyingine, kila jamaa akipiga simu anataka miadi ya kwenda kujirusha au kuvunja amri ya sita. Kama hilo silo unalotafuta, basi mtaalam anakushauri umtose jamaa haraka iwezekanavyo!

Taarifa za kukutana, ambazo ni za kushtukiza (Last minute get together): Mtaalam anasema, wakati mwingine katika mapenzi kushtukizana ni poa, ila ukiona mishtukizo ya kukutana inajitokeza mara kwa mara, basi ujue jamaa alikuwa na mipango ya kukutana na mtu mwingine, na baada ya mipango hiyo kwenda hovyo, anaamua kukupigia wewe. Kama unakumbuka ule usemi maarufu wa “tairi la spea”, basi ndio kinachoendelea hapo, mtaalam anasisitiza.Ukichanganya alama namba 2 na 3, jibu linaweza likapatikana kirahisi.

Hajifungi katika mpango wowote na wewe (Doesn’t commit to any plans with you): Hii alama inafanana na namba 3, isipokuwa alama hii inasaidia kuthibitisha alama namba 3. Kama mwanaume anamchukulia mwanamke kama “tairi spea” (chaguo la pili), hawezi kujifunga katika miadi ambayo itamuharibia mipango yake na lile chaguo la kwanza, mtaalam anaweka wazi

Hakutambulishi kwa marafiki/familia na facebook pia amebania: Kama mapenzi ndio kwanza yameanza basi usiwe na presha sana, lakini kama tayari mpo pamoja wiki 4 hadi 6, na bado haujakutana na jamaa yake yeyote, basi ujue hauna umuhimu sana kwake na ni wakati wa kuamua kusuka au kunyoa.

Mwisho wa siku, mtaalam anamalizia kusema kwamba lazima wakina dada muwe makini, kwani mnatakiwa mjue nafasi yenu katika maisha ya mwanaume ambaye umeanza nae mapenzi. Ni bora ukagundua nafasi yako mapema, kabla haujazama katika dimbwi la mapenzi (develop feelings), kwani ukishazama, inakuwa ngumu sana kujinasua.
 
Back
Top Bottom