MAALUM: Huddersfield yarejea ligi kuu, timu ya kwanza kushinda mataji matatu mfululizo Uingereza

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,690
239,249
Hii ni baada ya kuichapa Reading kwa mikwaju ya Penati 4 - 3, baada ya game kali sana ya Play off iliyopigwa Wembley na kumalizika kwa suluhu ya 0 - 0 katika dk 120.

Kila la heri Huddersfield Town
=====

Mwaka 1919 ikiwa ni miaka mitatu baada ya kuanzishwa, timu ya Huddersfield Town iliingia kwenye ligi kwa mara ya kwanza. Mwaka 1926 ikavunja rekodi kwa kuwa timu ya kwanza Uingereza kushinda mataji matatu mfulizo ya ligi Uingereza, rekodi ambayo imefikiwa lakini haijawi kuvunjwa. Huddersfield pia imechukua kombe la FA mwaka 1922 na kushiriki fainali nne za kombe hilo.

Mwaka 1932, mechi yake dhidi ya Arsenal kwenye kombe la FA ilivunja rekodi kwa kuhudhuriwa na watazamaji 67,037.

Baada ya vita ya pili ya dunia, klabu ilianza kushuka mfululizo na kutoka daraja la kwanza mwaka 1952 huku wakirejea miaka 14 baadae na kushuka tena baada ya misimu miwili.

Mwaka 1998, klabu ilimvutia mfanyabiashara kutoka mji huo, Barry Rubery na baada ya maongezi alichukua uendeshaji wa klabu hiyo akiahidi uwekezaji mkubwa. Hawakufanikiwa kurejea na kuangukia daraja la pili.

Rubery akaiuza kwa David Taylor na baadae Ken Davy. Mwanzoni mwa msimu wa 2004/05 kiwanja chake kilibadilishwa jina kwenda 'Galpharm Stadium' kutokana na udhamini wa kampuni ya afya.

Mwaka 2012 wakapanda mpaka championship baada ya mikwaju ya penati dhidi ya Sheffield United, mikwaju hiyo inajulikana kama mikwaju mirefu zaidi kwenye play-offs za ligi ambayo ilienda mpaka raundi ya 11 na matokeo ya mwisho kuwa 8-7.

Siku ya May 29, 2017 wataikumbuka kwa kurejea tena ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu 1972 wakimchapa Reading kwa mikwaju ya penati lakini safari hii ikiwa ya kawaida baada ya kushinda kwa mikwaju 4-3.
 
wombe moderators wabadili heading iwe Huddersfield special thread.

ili tuwe tunapata updates za timu hii makomne iliyo wahi kuchukua
ilianza lini n.k
Hawa jamaa wamechukua kombe la epl mara nyingi Zaidi ya spurs, spurs wamechukua mara 2 tu,So huddersfield > spurs
 
Back
Top Bottom