Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Hivi huyu Mkuu wa Mkoa wa Dar hao TAKUKURU hawajasikia tuu au hizi sheria kwa raia wa kawaida tu.
=====
Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imewaburuza kortini watu wanne akiwamo muuguzi mwandamizi wa Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi, anayedaiwa kugushi cheti cha shahada ya kwanza.
Muuguzi huyo, Hawa Nyanga alipandishwa kizimbani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Anthony Ngowi akidaiwa kughushi cheti kinachoonyesha kuwa amehitimu shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Texas Women cha nchini Marekani.
Waendesha mashitaka wa TAKUKURU wakiongozwa na Barry Galinoma akisaidiana na Caroline Lugenge na Furahini Kibanga, walidai kuwa Oktoba 17, mwaka 2011, Hawa alikiwasilisha cheti hicho na matokeo (Academic transcript) kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka hao wa TAKUKURU , muuguzi huyo aliwasilisha cheti hicho kinachodaiwa kuwa ni cha kughushi kwa RAS huku akijua si cha kweli, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu 342 na 337 cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Hata hivyo, mshitakiwa alikana mashtaka hayo na aliachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh3 milioni hadi Aprili 19 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa kwa mara nyingine mahakamani hapo.
Chanzo: Mwananchi