Bongo bwana unakuta mtu anajiita mdau wa sekta ya usafirishaji wakati hajawahi hata kumiliki toyota hiace nini lori au bus la yu-tong...
Moja ya tatizo la siku nyingi la Tanzania na watanzania ni kuacha kutumia akili kwenye matatizo ya msingi na hatimaye kupata suluhu baadala yake wanajikita kwenye kupiga ramli kwa kushirikisha watu wasio na ABC ya sekta husika au hata wale wenye uelewa mdogo..
Barabara nyingi za Tanzania zipo chini ya kiwango kiasi cha kuwa mtihani kwa watumiaji, ukosefu wa taa maeneo hatari usiku, sehemu nyingi kutokuwa na chaki nyeupe ya katikati, uzibaji viraka holela, mawimbi sehemu nyingi za barabara, kuwepo kwa kona zisizohitajika, madaraja mengi kukosa au kukaa muda mrefu bila kingo, uwepo wa vichaka sehemu za hatari..uwepo wa magari mabovu barabarani bila mamlaka kuchukua hatua..
Tanroad ni wakati wa kufanya kazi kisasa mkishirikiana na jeshi la polisi, mfunge camera kwenye baadhi ya Barabara kuu, kuwe na road patrol kila mkoa za polisi na tanroad kwenye barabara kuu kila siku mara kwa mara kuangilia kinachojiri barabarani, kila mkoa uwe na breakdown zitakazofanya kazi Barabara kuu, hizi breakdown ziwe na uwezo wa kuvuta malori makubwa yakiwa na mzigo pale yanapopata breakdown sehemu hatari yavutwe na kuwekwa sehemu salama ( mwenye gari lazima alipe hii chaji)..