Kwa hapa mimi nawalaumu wale wote walioajiriwa ku-maintain website ya bunge, pamoja na watanzania wote, haswa vijana wenzangu, wenye tabia ya uvivu uliokitihiri katika utendaji kazi mara baada ya kupata ajira. Bila kujali ajira hiyo imepatikanaje, tabia ya uvivu imetujaa sana vijana wa Tanzania, sijui tutatokaje hapa ila nadhani nchi yetu inapaswa ipate rais dikteta akayachapa watu viboko.
Niliwahi kuona "joke" fulani nadhani ilikuwa katuni, ikionesha muda wa kazi katika siku moja ya mfanyakazi serikalini, ilionesha kitu kama hiki:
Saa 2 asubuhi:Kufika kazini
Saa 2:30 kukaa ofisini
3:00 Chai
4:00-5:00 kugusagusa kazi
5: Kuingia Facebook and social media nyingine bila kusahau Whatsapp
6:00 Kuanza kupiga umbea na kusimulia yale uliyoyaona kwenye social media, tv na kwingineko, hapo wote mnasubiri saa saba ifike
Saa 7:00 Lunch time bana, kwani hujui? Utakujaje ofisini saa hizi
Saa 8:00 kurejea ofisini, kama boss yupo, vinginevyo saa 8:30
Saa 8:00 kugusagusa vikazi
Saa 8:30: Dah, usingizi unasumbua sana aisee, kusinzia kidogo
Saa 9:00: Duh, muda hauendi kabisa yaani, kusoma magazeti yaliyoletwa ofisini
Saa 10:00 Stori kuhusu watu waliofika kuhudumiwa hapo ofisini, yule sister....yule anko....yule mdingi.....
Saa 11:00 Oyaa, hivi nyie hamna saa au?? Jamani napata lift kwa nani leo?
Kwa ratiba hii, website mtu atahakikisha saa ngapi kuwa ipo updated or no? Halafu ai-update saa ngapi? Ile barua yako uliyotuma eti unasubiri majibu, saa ngapi itasomwa halafu bosi apelekewe atoe ushauri halafu uandikiwe majibu, yapelekwe posta ili uyapate??
Mtazamo wangu.