Maajabu 2017 Kijana (18) ageuka mtoto ghafla tazama picha

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,526
51,216
Maajabu ya Mwaka 2017..Kijana Miaka 18 Ageuka ‘Mtoto’ Ghafl

Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushangaza, wananchi wa Kijiji cha Rokili, Halimashauri ya Wilaya ya Siha mkoani hapa, wapo kwenye mshangao kufuatia tukio la Kennedy Josia Nkini (18), kukumbwa na ugonjwa wa ajabu uliomsababisha kuwa mfupi ghafla.

Akizungumza na Gazeti la Amani juzi, mama mzazi wa mtoto huyo, Mary ambaye pia ni mgonjwa, alisema mwanaye alizaliwa mwaka 1999 akiwa mzima wa afya ambapo aliendelea kukua vizuri hadi alipofikisha umri wa miaka 11 (2006), kipindi hicho akiwa mrefu tu, akaanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Rokili iliyopo Siha.

Mama huyo alisema familia ni ya watu warefu sana hivyo mwanaye akiwa na miaka 10 tu tayari alikuwa mrefu, sasa katika hali ya kushtua, siku moja mwanaye aliporudi shule alianza kunyonyoka nywele kichwani na kuwashwa na kila alipojikuna nywele zilitoka. “Nilimuuliza labda ameiba maparachichi ya watu shambani akakataa, akasema hali hiyo ilimtokea ghafla.

Ndipo nilipompeleka Hospitali ya KCMC Moshi ambako alilazwa kwa ajili ya uchunguzi. “Siku iliyofuata asubuhi, niliitwa chumba cha daktari na kuulizwa mtoto wangu alikula chakula gani? Nikawaambia sikumpa chochote, wakanipeleka kumshuhudia.

“Nilipigwa butwaa baada ya kumuona mwanangu. Hakuwa tena yule niliyeingia naye usiku wa jana yake, alikuwa mfupi kupita kiasi. Nilishangaa sana. Nikaangua kilio nikiwauliza madaktari kulikoni mwanangu amekuwa vile?

24fc178d2a2e1e1c3627b7ac40b7f2ec.jpg
Na wao hawakujua kilichotokea,” alisema mama huyo. Mama huyo alisema, mtoto wake aliendelea kulazwa KCMC miezi nane akimuuguza ambapo tayari ngozi yake ilikuwa imebadilika na kuwa na magamba kama ya mnyama, miguu ikizidi kuwa midogo kama ya mtoto na kukosa nguvu ya kutembea.
fb03d27955416fd0f384e72bcd8a4c85.jpg

Alisema madaktari walijitahidi kumsaidia mtoto huyo lakini ikashindikana, hatimaye walimruhusu kuondoka naye kwa ajili ya kwenda kujaribu dawa za miti shamba ambazo pia hazikumsaidia.

Mama alisema, licha ya Kennedy kuwa hivyo, waliona aendelee na shule lakini na yeye mtoto licha ya maumivu makali, alipenda kusoma hivyo waliongea na walimu wa shule na kumruhusu kuendelea kusoma licha ya kwamba kulikuwa na hali ya kutengwa na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walikuwa wakimuogopa.

“Baba yake anaitwa Josia Zefania Nkini ana miaka 59, alipata kazi ya ziada ya kumbeba mgongoni kumpeleka shuleni umbali wa kama kilomita tatu na alitakiwa kumpeleka asubuhi na jioni kumfuata hadi alipomaliza darasa la saba mwaka jana na kufanikiwa kufaulu.

Hapa anatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.” Kijana huyo amefaulu kutoka Shule ya Msingi Rokili ambayo ipo mlimani lakini sekondari aliyopangiwa kwenda ni ya Suumu, pia ipo Halmashauri ya Siha na ipo mlimani juu kabisa ambapo kwa hali aliyonayo itakuwa ndoto kufika huko.

Kilio cha majirani, familia ya kijana mwenyewe ni kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick wamsaidie kumtafutia shule itakayoendana na hali yake.

Amani lilifanikiwa kuongea na kijana Kennedy ambaye licha ya hali yake lakini yeye anaona kawaida na anajichukulia kama binadamu wengine na ni mcha Mungu kwani hata Amani mara baada ya kufika nyumbani kwao, kabla ya mazungumzo alianza kumpa Mungu utukufu kwa kusali ndipo maongezi yaliendelea.

3114c2afced625dcfa05ed6c538e1091.jpg

Alisema: “Kaka mimi nimeshakubaliana na hii hali ya ulemavu ingawa bado nina tumaini siku moja Mungu anaweza kuniokoa na nikarejea kama zamani pamoja na urefu wangu, lakini kinachonipa mawazo muda mwingi ni kuhusu kusoma.

Napenda sana kusoma ndiyo maana hata darasani nimekuwa mtu wa kumi na kufanikiwa kufaulu.”

“Naiomba serikali kupitia kwa waziri wa elimu inisaidie kunipatia shule ya walemavu, lakini nguo sina, baiskeli yangu imeisha, matairi yalishapasuka mwaka wa tatu sasa na mama yangu anaumwa mwaka wa pili huu,” alimaliza kusema.
 
Oh My God
Mung atakusaidia mdogo wangu pole sana naamin utaendelea kusoma.Naamin kilio chako kitafika sehemu husika ili uweze kupata msaada wa haraka. Naomba Endelea kumtumain Mungu ivo hivo.
 
dah nilitaka nisiamini kwa vile hii habari imeandikwa na gazet la udaku lakin nahis ni kweli.. .pole kijana mungu atakusaidia
 
Nilipoona ni gazeti la Amani ndo lenye habar hii nikaacha na kusoma
 
Mungu ni mwema... hakuna lisilomshinda yy.
Ee Mungu uishie mahala juu mbinguni mwangalie huyu mtoto wako kwa huruma.
Mfariji na mrudishie afYa yake ya awali.
Amen
 
Mungu ni mkubwa ahimidiwe milele..
mimi ndio siwaelewi ama nyie nfo mmeandika chafs?,Mungu hapa ahimidiwe kivipi?kwa kumfanya mtoto kuigua ama?Kwani mungu alikua wapi mpaka mtoto kua katika hali kama hii kiasi kwamba sasa hi i ndo mnamkumbusha mungu majukumu yake aliyotakiwa kuyafanya kabla ya tukio?.Au alijisahau?

Hiki kizazi cha ajabu sana

.......Free ideas......
Mungu ahimidiwe

eee Mungu saidia.....

Oh My God
Mung atakusaidia mdogo wangu pole sana naamin utaendelea kusoma.Naamin kilio chako kitafika sehemu husika ili uweze kupata msaada wa haraka. Naomba Endelea kumtumain Mungu ivo hivo.
 
mimi ndio siwaelewi ama nyie nfo mmeandika chafs?,Mungu hapa ahimidiwe kivipi?kwa kumfanya mtoto kuigua ama?Kwani mungu alikua wapi mpaka mtoto kua katika hali kama hii kiasi kwamba sasa hi i ndo mnamkumbusha mungu majukumu yake aliyotakiwa kuyafanya kabla ya tukio?.Au alijisahau?

Hiki kizazi cha ajabu sana

.......Free ideas......
Ask God those questions of yours. Dont overload us with your questions which you know perfectly you can go and ask God about it. We just point out our views. Dont provoke yourself over nothing.
 
Show me your god so that i may ask him/her/it
 
Kaka unapoteza Muda kufanya arguments ambazo MUNGU anaziita mizaha.. Unazid kujaza junks kwenye brain vitu visivyo na mantiki.. Yeye yupo kwenye kundi LA wasio amini uwepo wa MUNGU.. Lakini ukiwauliza origin ya Ulimwengu hawaijui vizuri watakupa theories nying Ambazo pia na zenyewe zina mapungufu mengi na unanswered questions
 
Show me your god so that i may ask him/her/it
"Heri wamchao Bwana mana ufalme wa Mbinguni ni wao"

Siwezi kubishana na mtu asieamini, huamini Mungu yupo na huamini matendo makuu ya Mungu, kuna haja gani kukuambia ama kukuelewesha ili na wewe umuone kupitia neno lake na matendo yake, au ulifikiri unamuona live?! Let me save my breath.
Kwaheri.
 
Back
Top Bottom