Maafa ya MV Nyerere Ukara

El'son

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2012
Posts
380
Reaction score
324
Ndugu zangu watanzania kwanza niwape pole kwa maafa yaliyotokea juma lililopita. Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu sana. Nimejaribu kuvumilia lakini nimeona isiwe tabu hebu tujadili hili kwa kirefu zaidi.

Binafsi nimekaa nikatafakari sana kuhusu hii ajali ya MV Nyerere kwa namna ilivyoleta maafa makubwa miongoni mwetu, lakini mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi, japo siwezi kupingana hali halisi tayari vifo vimeshatokea kwa watanzania wenzetu.

Kikubwa kinachonishangaza ni ukaribu wa eneo la ajali ilipotokea na maafa yaliyotokea. Ni vitu ambavyo havioani kabisa. Kama ajali hii ingetokea zaidi ya kilomita kadhaaa basi hii hoja yangu isingekuwa na mashiko. Lakini ukiangalia picha ya mazingira ya ajali utaona ajali imetokea ndani ya mitaa kadhaa tu. Na ukilinganisha mita hizo na idadi ya watu waliokolewa unaweza pata kizunguzungu. Ajali hii imetokea karibu sana jamani mtu yupo ufukweni anaona kabisa kila kitu, sasa nini kimetokea mpaka idadi ya waliokufa iwe kubwa kiasi hicho. Kwa mazingira hayo nilitarajia watu wengi zaido ndio wangeokolewa.
Najaribu kutafakari tuu ila bado nashindwa amini. Niwatakie tafakuri njema ndugu zangu.
 
Mkuu kivuko kilipinduka.... Yaani ile buu bah...!!!! Waliosalimika ni kama vile walitupwa kwenye maji wakati kinapinduka... Kingezama kawaida si ajabu wote wangepona.
 
Mkuu kivuko kilipinduka.... Yaani ile buu bah...!!!! Waliosalimika ni kama vile walitupwa kwenye maji wakati kinapinduka... Kingezama kawaida si ajabu wote wangepona.
Kweli kabisa, kingezama wangeokoka wengi maana wakazi wengi wa kule bila shaka wanajua kuogelea vizuri tu!
 
Hapo mm mwenyewe nakosa majibu kabisa, ila nahisi hao waliokolewa ni wale ambao walirukia kwenye maji na wakaonyesha jitihada za kujinasua ndio wakasalimika. Hao wengine nadhani walibakia humo humo ndani ya kivuko hadi mwisho kilipoamua kuwafunika nadhani walikosa pa kutokea ndivyo ninavyohisi. itakuwa kilienda chini na kikafunika watu wote, mfano mende umemfunika na bakuri nadhani anakosa pa kwenda anabakia hapohapo....ndio maaana waziri mkuu pia akasema inawezekana ikapatikana miili mingi zaidi baada ya kivuko kunyenyuliwa. Hata wao wanahisi hivo.

NB: usisahau kuwa huwa tunaaswa kutokuruka wakata wa ajari, badala yake kushikilia mahali ambapo utasubiri hadi ajari ikatulia kabisa, nadhani nao walizingatia hilo na kujisahau kuwa mle ni kwenye maji haikutakiwa kukomaa na mabati badala yake ilikuwa kujirusha kwenye maji. Waoga wa kuogopa mamba, ama kutokujua kuogelea ndio wengi wameangamia humo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…