Katika dunia ya leo, ili uishi maisha ya amani inabidi upambane na maadui watatu.
1. Nyumba ya kupanga. Huyu ndio adui namba moja. Bora hata uishi kwenye dungu la tope la kwako mwenyewe kuliko kero za kuishi nyumba ya kupanga.
2. Kutumia usafiri wa umma. Hii ya kila siku kunukishana vikwapa kwenye daladala na kero nyingine za vyombo vya usafiri wa umma ni adui namba mbili.
3. Kuajiriwa. Baada ya kero za mwenye nyumba, kero ya usafiri wa umma mwishowe ni hii kero yakuajiriwa. Hasa unapokuta IQ yako kubwa halafu wanaokuongoza wana IQ ndogo. Ndio shida inapoongezeka.
Siku zote tupambane kuwatokomeza maadui hawa watatu.
Mkuu,
1. Unamaanisha nyumba ya kupanga au makazi?
2. Kutumia usafiri wote wa umma?
3. Kuajiriwa au Kutegemea kipato cha kuajiriwa?
Unaposema maadui watatu wa Mwanadamu, unamaanisha "maadui" watayu wa mtanzania au, kwasababu si wanadamu wote wenye kuishi katika nyumba za kupanfa lakini huishi katika maisha mazuri! Na wapo waishio katika nyumba zao lakini ni bora wangepanga.
Kuna nchi ambazo ni gharama sana kujenga! Nchi ambazo kwa watu wanaoishi mijini kupata eneo!
Pili, kuna watu waishio katika maeneo ya mbali ambapo ni usafiri wa umma mf. treni, mabasi ndiyo pekee suluhisho. Sasa unaposema hili nalo ni adui, iweje kwa mtu akaaye km 50+ ambaye hawezi kutumia usafiri wake wa binafsi ingawa anao?
Tatu, issue sidhani kama ni kuajiriwa..nadhani kutegemea kipato kimoja cha kile ulichoajiriwa ndiyo shida! Kwa dunia ya sasa, si rahisi (ingawa inawezekana) kutegemea kipato kimoja unless kuwe na rushwa au wizi. Lakini, je ni wote wataweza kujiajiri?
So, binafsi sioni kama hawa ni maadui wa 'mwanadamu', unless tujue mwanadamu huyu yuko katika mazingira yapi/gani! I stand to be corrected.