Lyatonga Mrema: sijaona mgombe urais kama Magufuli

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Wana JF,

Huyu Mwenyekiti wa Bodi ya Parole na Mwenyekiti wa chama cha TLP ndo ameshakiua chama chake au hali ya maisha ndio inamfanya aongee anacho kisema.

Leo kwenye dka 45 ITV mzee amesema kuwa wakati wa kampeni ya mwaka 2015 aliangalia akaona hakuna mtu mwenye uwezo wa kuiongoza nchi kama Magufuli, chama chake kilimsimamisha mgombea wa urais sasa sielewi ali mdharau na kuwadharau wanachama wake waliopiga kura kwenye chama ya kuwa na imani na mgombea wa TLP na hivyo kumruhusu agombee kwa nafasi ya urais.

Hivi inaweza ikatokea kwa mwenyekiti wa chama kumnadi mgombea urais wa chama pinzani huku mkijua mnaye wa kwenu? Naomba mnisaidie kujua kuna nini kwenye brain yake. Sasa hivi kwenye TV anamsifu na kumtetea Magufuli kwa nguvu zote haja taja hata kitu chochote kinachohusu chama chake huyu mzee anashida gani, pesa imeshampoteza nahisi TLP haitakuwepo tena kwenye ramani ya vyama maana kama mwenyekiti ndo hivi alivyo poleni wana TLP.
 
Back
Top Bottom