Lwakatare: Tetemeko la ardhi Bukoba

Dec 10, 2015
22
70
HABARI YA JUMAPILI NDUGU WANA WA BUKOBA NA MKOA KAGERA KWA UJUMLA.

Nawasalimia na kuwapa pole kutokana na mtikisiko wa tetemeko la ardhi uliojitokeza kwa mara nyingine usiku wa kuamkia leo.

Tumshukuru kwa pamoja mwenyezi Mungu kwamba hakuna madhara makubwa zaidi ya mishtuko ya nafsi zetu, kwa kumbukumbu ya maafa yaliyotukuta Sep 10 2016.

Kwa pamoja tuzidi kumuomba mwenyezi Mungu atuepushie majanga na madhara makubwa yanayoweza kutokana na tetemeko la ardhi.

Pia tuendelee kuwa wavumilivu, waangalifu na kuhimili hofu zetu. Kwa mujibu wa wataalamu wa mazingira (Geologists); mitikisiko midogo midogo itaendelea kujitokeza kwa miezi 6 baada ya tetemeko kubwa la Sep 10 2016.

Niwasii sana wanaBukoba na mkoa Kagera kwa ujumla kuhudhuria sherehe za wiki ya msalaba mwekundu duniani ambapo kitaifa zitafanyika mkoani kwetu Kagera ndani ya Manispaa ya Bukoba kuanzia tarehe 01/05/2017.

Msalaba mwekundu (Red cross) wamekuwa pamoja nasi tangu majanga ya tetemeko la ardhi na mafuliko ya mto Kanoni hivi karibuni, hivyo kwa kutambua mchango wao na ujuzi wao katika uokozi na huduma ya kwanza, ni wito wangu kwa wananchi wenzangu tujitokeze kwa wingi ili tupate mafunzo stahiki kwa ajili ya kujikinga na kujiokoa wakati wa majanga.

Nitakapokamilisha kazi ya kuwawakilisha kama mlivyonituma kwenye vikao vya bunge, hima nitarejea jimboni kuungana na kikosi kazi cha Manispaa ya Bukoba kinachoongozwa na Mstahiki Meya Chief Kalumuna kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani, watendaji wa halmashauri chini ya UKAWA kupambana kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya jimbo letu kama tulivyohaidi.

NAWATAKIA SIKU NJEMA, UPENDO NA AMANI VITAWALE.

Wilfred Lwakatare (MB)
 
Hapo kwenye 'kuhimili hofu' unamaanisha nini? Kweli kuna anayeweza kuhimili hofu ya tetemeko la ardhi hivi hivi? Kwa taarifa yako mheshimiwa hofu ya tetemeko hukabiliwa kwa alert. Yaani watu wapewe taarifa mapema kuwa tetemeko lisilo na madhara makubwa litapita muda fulani. Hivyo watu wanakuwa tayari muda huo. Shirikiana na watalaamu wakupe namana bora ya kuwafanya wananchi wako wasiwe na hofu ya tetemeko.
 
Asante sana ,na tunamshukuru mwenyezi kwani pamoja na tetemeko kutikisa usiku lakini had I sasa hakuna madhara yaliyoripotiwa.
 
Kwa sasa wana Bukoka watakuwa wamesha ji-tune na wanaweza kukabiliana wenyewe na changamoto za matetemeko ya mara kwa mara maana wanajua kama wakitegemea serikali wataishia kuoata fedheha. Poleni sana wana Bukoba
 
Back
Top Bottom