Lusinde aiponda serikali

Lusinde aiponda serikali

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,290
Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya (CCM), Livingstone Lusinde amefunguka na kuiponda serikali kuwa inashindwa kusimamia mambo yake vizuri jambo ambalo linapelekea matumizi ya fedha kuwa makubwa huku miradi ikikwama.

Lusinde.jpg

Lusinde amesema hayo leo bungeni wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa serikali imekuwa ikishindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha jambo ambalo linazidi kuturudisha nyuma kimaendeleo.

"Waziri akinisikiliza vizuri anaweza kuona namna ambavyo serikali wakati mwingine inashindwa kusimamia matumizi mazuri ya fedha kwani ikisimamia vizuri fedha thamani ya fedha itaonekana na tutapata maji mengina kwa uhakika kwa mfano watu wa WFP wametupa milioni mia saba tisini na tisa kwenye jimbo la Mtera kwa fedha hizo hizo tumepata matenki makubwa ya lita laki nane matatu, tumepata visima kumi na nane, tumepata mashamba heka mia tatu kwa ajili ya umwagiliaji, tumepata visima kumi na mbili vilivyofungwa solar Power kwa ajili ya wananchi kupata maji hebu angalia matumizi haya ya fedha hizi yameleta vitu vikubwa ambavyo wananchi wananufaika lakini ukija kwenye serikali hakuna kitu"

"Kwenye serikali inatolewa bilioni moja pale Kwayungu kwa ajili ya kujenga bwawa la umwagiliaji mpaka sasa bwawa halijakamilika, hakuna miundombinu na bilioni imeliwa kwa hiyo unaweza kuona matumizi mabaya kwenye miradi ya maji kwa upande wa serikali ndiyo yanatuletea matatizo makubwa hawa wametoa milioni 800 wametengeneza mambo ambayo ni maajabu kabisa, Mhe Waziri na Katibu Mkuu piteni muone namna ambavyo pesa ikisimamiwa hata ikiwa kidogo inaweza kufanya vitu vikubwa watu saizi wanapata maji ya kunywa, wanamwagilia na maisha yao yapo safi" alisisitiza Lusinde

My take:
Mi naona huyu jamaa kacheza na uelekeo wa spika wa bunge huyu haaminiki kacheza na mdundo wapi upepo unavuma huyu ni bendera fuata upepo.
 
Dah! At long last jamaa angalau anainyooshea kidole na kutofautiana na serikali ya chama chake!
 
Huyo nna hakika na yy ana Hakka hawezi kuwepo kweny bunge 2020
 
Ccm Kule anakokwenda bwana mkubw na wao hufuatia. Hiyo ni bosheni tu kutuzuga.
 
Paka jike anamlaumu paka dume kuwa hawatendei haki panya.

NI mwehu tu ndiye atajayemuamini.
Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya (CCM), Livingstone Lusinde amefunguka na kuiponda serikali kuwa inashindwa kusimamia mambo yake vizuri jambo ambalo linapelekea matumizi ya fedha kuwa makubwa huku miradi ikikwama.

Lusinde.jpg

Lusinde amesema hayo leo bungeni wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa serikali imekuwa ikishindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha jambo ambalo linazidi kuturudisha nyuma kimaendeleo.

"Waziri akinisikiliza vizuri anaweza kuona namna ambavyo serikali wakati mwingine inashindwa kusimamia matumizi mazuri ya fedha kwani ikisimamia vizuri fedha thamani ya fedha itaonekana na tutapata maji mengina kwa uhakika kwa mfano watu wa WFP wametupa milioni mia saba tisini na tisa kwenye jimbo la Mtera kwa fedha hizo hizo tumepata matenki makubwa ya lita laki nane matatu, tumepata visima kumi na nane, tumepata mashamba heka mia tatu kwa ajili ya umwagiliaji, tumepata visima kumi na mbili vilivyofungwa solar Power kwa ajili ya wananchi kupata maji hebu angalia matumizi haya ya fedha hizi yameleta vitu vikubwa ambavyo wananchi wananufaika lakini ukija kwenye serikali hakuna kitu"

"Kwenye serikali inatolewa bilioni moja pale Kwayungu kwa ajili ya kujenga bwawa la umwagiliaji mpaka sasa bwawa halijakamilika, hakuna miundombinu na bilioni imeliwa kwa hiyo unaweza kuona matumizi mabaya kwenye miradi ya maji kwa upande wa serikali ndiyo yanatuletea matatizo makubwa hawa wametoa milioni 800 wametengeneza mambo ambayo ni maajabu kabisa, Mhe Waziri na Katibu Mkuu piteni muone namna ambavyo pesa ikisimamiwa hata ikiwa kidogo inaweza kufanya vitu vikubwa watu saizi wanapata maji ya kunywa, wanamwagilia na maisha yao yapo safi" alisisitiza Lusinde

My take:
Mi naona huyu jamaa kacheza na uelekeo wa spika wa bunge huyu haaminiki kacheza na mdundo wapi upepo unavuma huyu ni bendera fuata upepo.
 
Kuna kitu wameshajadili kichama...........msikubali kuchotwa akili

UTABIRI
Baada ya muda mfupi kuna mtu atatumbuliwa kwa kisingizio cha kufuata maazimio na ushauri wa wabunge.
 
Uko sahihi mkuu.
 
Back
Top Bottom