Lukuvi: Hekari 30 mjini zote za nini?

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
635
LUKUVI -
“Utakuta mtu anamiliki ekari 30 mjini, zote hizo za nini, utafika wakati tutawazuia kuuza maeneo hayo kwa sababu wanaiibia Serikali,” alisema Lukuvi.

LUKUVI ATANGAZA KITANZI KWA MADALALI WA ARDHI
Na MAREGESI PAUL-DODOMA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema Serikali inatarajia kuandaa sheria itakayowabana madalali katika sekta ya ardhi.

Amesema lengo la sheria hiyo ni kuwabana madalali hao ambao wamekuwa wakiuza ardhi katika siku za mapumziko kutokana na sababu wanazozijua wao.

Lukuvi aliyasema hayo bungeni jana alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Wizara hii itatunga sheria ya kuwadhibiti madalali wanaowaonea wananchi kwa kuuza nyumba siku za sikukuu na weekend. Hao kiama chao kinakuja kwa sababu tutawatungia sheria na tutawatambua kwa sifa zao kisheria.

“Hata wenye maeneo makubwa mijini, lazima tutaanza kuwatambua na kuwatoza kodi hata kama hawajayapima.

“Utakuta mtu anamiliki ekari 30 mjini, zote hizo za nini, utafika wakati tutawazuia kuuza maeneo hayo kwa sababu wanaiibia Serikali,” alisema Lukuvi.

“Katika hilo, Serikali imejipanga kuhakikisha kila ardhi iliyopo nchini, inapimwa na kutumika kwa usawa na haki kama ilivyokusudiwa kwani kuna watu wanatakatisha fedha zao kupitia sekta ya ardhi,” alisema Lukuvi.

Kuhusu utoaji wa miliki za ardhi, alisema wizara yake itaendelea kushirikiana na halmashauri na sekta binafsi kuhakikisha kila ardhi inapimwa na kumilikishwa.

“Katika mwaka wa fedha 2016/17, wizara iliahidi kuandaa hatimiliki za ardhi 400,000 na kutoa hati za hakimiliki za kimila 57,000.

“Hadi kufikia Mei 15 mwaka huu, wizara imetoa hatimiliki za ardhi 33,979 na imeratibu uandaaji wa hati za hakimiliki za kimila 35,002 na pia wizara imeandaa vyeti vya ardhi za viijiji 505.
“Lakini, katika mwaka wa fedha 2017/18, wizara yangu kwa kushirikiana na halmashauri nchini, itaandaa hatimiliki za ardhi 400,000, vyeti vya ardhi ya vijiji 1,000 na kutoa hati za hakimiliki za kimila 57,000.

“Ili kuwawezesha wananchi wengi kupata hatimiliki za ardhi, wizara inakusudia kupunguza tozo ya mbele ambayo hutozwa wakati wa kumilikisha kutoka asiliia 7.5 mpaka asilimia 2.5 ya thamani ya ardhi.

“Kwa hiyo, natoa wito kwa halmashauri zote nchini, kuhakikisha zinamilikisha viwanja vyote vilivyopimwa na kuandaa hati ili wananchi waweze kuwa na miliki salama,” alisema Lukuvi.
Wakati huo huo, alisema wizara yake itaendelea kuhakiki viwanja na mashamba nchini ili kubaini ukiukwaji wa masharti ya umiliki .

Pamoja na hayo, alisema baada ya kufanya uhakiki siku zilizopita, wizara yake imeshabatilisha miliki za viwanja 227 na mashamba 17 kutokana na ukiukwaji wa masharti. Viwanja na mashamba hayo, viko katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Iringa, Kagera na Morogoro.

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alimtaka Waziri Lukuvi atakapoanza kuchukua hatua kwa waliokiuka sheria za ardhi, asiangalie itikadi za kisiasa na badala yake kila mmoja achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu mradi wa viwanja 20, 000 jijini Dar es Salaam, aliitaka Serikali ifanye uhakiki wa viwanja hivyo ili kujua uhalali wa viwanja hivyo.

Pia, alitaka sheria za kimila za umiliki wa ardhi zinazowakandamiza wanawake, alitaka ziangaliwe upya ili wanawake nao wawe na haki ya kumiliki ardhi kama walivyo wanaume.

Naye Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM), alitaka migogoro ya ardhi inayohusisha wananchi na maeneo ya jeshi, itatuliwe haraka ili wananchi waishi kwa amani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF), alilalamikia bei ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na kusema zinauzwa kwa bei kubwa ingawa viongozi wa shirika hilo wamekuwa wakisema zinauzwa kwa bei ndogo.

Chanzo: Mtanzania
 
Lukuvi mwenyewe ana bonge la gorofa mjini kalijenga kwa bilioni kadhaa....gorofa lote hilo la nini na pesa ametoa wapi? atakuwa ni mmojawapo wa wanaoiibia serikali
Kwa hiyo hilo hekalu limekamata eka 30?
Uskurupuke.!
 
Ekari 30 kama ni Mtanzania ni haki yake. Ni hivi Lukuvi, wawekezaji uchwara ndio unapashwa kukimbizana nao waacheni Watanzania waneemekeeee kha kila siku vitisho ilimradi kuwakosesha amani watu.
 
Ekari 30 kama ni Mtanzania ni haki yake. Ni hivi Lukuvi, wawekezaji uchwara ndio unapashwa kukimbizana nao waacheni Watanzania waneemekeeee kha kila siku vitisho ilimradi kuwakosesha amani watu.
Hapo sasa

Mtu kajidunduliza badala ya kutafuta namna ya kumsapoti wanampiga biti
 
Huyo aliyezungumzia bei za nyumba za NHC aungwe mkono. Utaratibu wa kuzinunua unavutia sana tatizo bei tu. Halafu wafikirie na namna nyingine sio lazima kila siku wajenge nyumba zilizoshikana utafikiri mabanda ya njiwa
Hahahaha mabanda ya njiwa
 
Kwa hiyo hilo hekalu limekamata eka 30?
Uskurupuke.!

Think outside your skull, kwanini asiwe na nyumba ya vyumba viwili tu? ni hivi mwenye ardhi ndio kaweza kuwa na hiyo akaamua kuwa na heka 30 kuna tatizo gani? mbona kuna watu wana nyumba 700 tatizo liko wapi? kwanini wasiwe na moja tu? Kwanini watu wana wake 10, kwanini asiwe na mmoja tu? maswali ni mengi kwa logic hiyo.... kwa kifupi wewe na yeye mnachemka tu kuuliza swali kama hilo....
 
Huyo aliyezungumzia bei za nyumba za NHC aungwe mkono. Utaratibu wa kuzinunua unavutia sana tatizo bei tu. Halafu wafikirie na namna nyingine sio lazima kila siku wajenge nyumba zilizoshikana utafikiri mabanda ya njiwa
Kijiji cha ujamaa na kujitegemea!
Hahahaha, hakuna kuchekana, ila nafikiri ukinunua waruhusiwa kuzibadilisha, maana ziko kama uniform za shule aise..
 
Lukuvi anadai kwani kuna ubaya gani kuwa na vihekari 2 au vitatu kutokana na watoto ulio nao, ziendeleze, sasa hekari 30, kuendeleza issue, lawa pori, wezi majambazi guest humo humo, bila kusahau nyoka na wadudu wabaya, labda tujaribu kumuelewa..maana hekari 30 si mchezo kaka..
 
Lukuvi mwenyewe ana bonge la gorofa mjini kalijenga kwa bilioni kadhaa....gorofa lote hilo la nini na pesa ametoa wapi? atakuwa ni mmojawapo wa wanaoiibia serikali
Upo nyuma sana mkuu.
Siku hizi ukiwa na hati unapata mkopo wa uenzi 100% kutoka benki haswa BOA Bank
Ni rahisi sana kwa mtu mwenye dhamana ya uwaziri kukopa kuliko wewe kajamba nani,hivyo usione ajabu kwa Lukuvi kuwa na ghorofa,ile kodi ya pango itakwenda benki moja kwa moja kufidia deni.Deni likiisha anarudishiwa hati yake
 
Ila binadamu balaa, kujilimbikizia mahekari 30 yote ya nini? Kwani watoto nao hawatatafuta?! Wape elimu na matunzo bora kwishnei, sasa mahekari, maghorofa, mahela benki, magari, manyumba! usishangae mitoto ikauza yote hayo, au ikawa maugomvi ya kufa mtu, kisa urithi, au ikawa mivivu isitafute kabisa, waachie kajumba kamoja kama "Headquarters", zaidi hayo niliyotaja juu, mchezo kwisha nawo wapambane..
 
Nawatoto 20, wake 4, wajukuu 6 na vimada 4, mkuu hizo 30 hazinitoshi niongezee nne mkuu.
 
Back
Top Bottom