Lowassa Kurudi "Nyumbani" - Mtazamo Chanya

B.Louis

Member
Joined
Aug 5, 2009
Posts
81
Reaction score
38
Natumaini mko salama wanajamii. Napenda kujumuika na Watanzania wengine wengi ambao wameshaandika kuhusu siasa zetu kama taifa na jinsi zinavyokanganya hasa wale wenye taarifa finyu, wasio na uwezo mkubwa wa kuchambua yanayotokea katika medani za siasa na wachanga katika nyanja za siasa. Inasikitisha lakini kuna matumaini.

Binafsi nilishangaa sana kuona Bwana Lowassa amekatwa jina lake pale Dodoma miaka kadhaa iliyopita ambapo Mh. Rais wa sasa Dr. JPM alipita kwa kishindo. Wakati fununu zilipoanza kutawala kwamba hatapitishwa pamoja na "mafuriko" ya wana CCM aliyokuwa akiyasababisha, nilidhani ni propaganda. Na pale ambapo kukatwa kwake kulitanabaishwa kwamba kutatokana na uhusiano uliozorota kati yake (Lowassa) na rafiki yake ambaye kwa mujibu wake yeye mwenyewe "hawakukutana barabarani", Mh. Rais wa wakati huo Dr. JMK.

Kwanini nilidhani ni propaganda? Sababu ya kwanza ni kwa sababu pamoja na madhaifu yake yote yaliyokua yakisemwa kipindi kile kwamba ni "mchafu" sana na hivyo hasafishiki, itakua ngumu sana kumuuza kwa wapiga kura na mengine kama hayo; mafuriko yake yalidhihirisha kinyume na yaliyokuwa yanasemwa. Na kwa kua mtaji wa kisiasa ni watu basi hakika alikua nao wa kutosha.

Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja aliniambia Mh. JK atamkata tu kwa sababu ya tofauti zao binafsi, na kwa mujibu wake ndio sababu ya kumuachia jumba bovu la Richmond kumuangukia na hatimaye kulazimu ajiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu. Lakini bado kwa utashi wa kawaida wa kisiasa na hii ndio sababu ya pili, ilikua rahisi zaidi kusuluhisha tofauti hizo binafsi kuliko vinginevyo. Na yaliyotokea sote tunayajua. Hakuna wakati ambao upinzani umepata viti vingi na kura nyingi kama katika uchaguzi wa 2015.

Nije sasa katika hili la kurejea "nyumbani". Siwezi semea sana hali za CCM wala CHADEMA za ndani kwani sizifahamu. Lakini kwa nje CCM inatawala na CDM iko katika hali ngumu sana pengine tangu kuanzishwa kwake. Kesi mahakamani, jela kwa viongozi wake, na mengine mengi kwa uchache na tunayoyasoma kwenye vyombo vya habari na mitandaoni. Lowassa kwa kuwepo CDM ameona kwa vitendo madhara na faida za kuwa mpinzani. Kwa kifupi Mtawala analindwa na sheria kuu mbili ambazo hata kama sheria nyingine zote zikivunjwa lakini hizi mbili zitahalalisha uvunjwaji huo.

Sheria ya kwanza ni ya kutomshitaki Rais popote kwa lolote alilolifanya akiwa madarakani na hata akishaondoka(Ibara ya 46 ya katiba ya JMT). Na ya pili ni ya kutopinga matokeo ya uchaguzi ya Urais popote, ndani au nje ya nchi, yakishatangazwa na tume ya uchaguzi(Ibara ya 72 ya katiba ya JMT) Hata Lowassa angehamia upinzani na nchi nzima mambo ya "Jecha" yangeweza kutokea pia. Lakini mamlaka ya Rais yangeweza kutumika kubadili chochote ambacho kisingempendeza JK wakati ule na pasingekua na mahali pa kupinga wala kuhoji maamuzi yake. Na alisema pale Lumumba mbele ya wana CCM kua "mwali" anaye yeye hivyo wasiwe (wana CCM) na wasiwasi.

Kurudi kwa Lowassa CCM, anarudi akijua haya. Anayajua kwa vitendo mtambuka kama mpinzani....Rais akisema ni sheria. Lakini pia kimtizamo kwa maana ya upinzani si uadui. Mpinzani ni Mtanzania pia kama alivyokua yeye. Pia ametambua utu, umakini na heshima aliyopewa alipoenda upinzani. Kwa kifupi Lowassa anayerudi CCM sasa hivi si yule aliyeondoka. Huyu kaonja mahakama, kuitwa polisi kwa mahojiano na mengine mengi. Huyu wa leo anaweza akashauri na kushawishi mabadiliko ya katiba na sheria zile mbili zikafungua ukurasa mpya katika siasa na demokrasia ya Tanzania bila kujihisi anasaliti chama chake cha sasa wala watawala waliopo na waliopita.

Warioba hakuweza kwani yeye mwenyewe na waliomtuma hawakuona na pengine hawaoni aliyoyaona na anayoyaona Lowassa. Na ndani ya CCM kukiwa na ufahamu kwamba hata kama JPM angekuwa anatoka upinzani angetawala hivi hivi anavyotawala sasa kwa mujibu wa sheria zilizopo, wana-CCM wasingeng'ang'ania kupiga vita upinzani. Binafsi nina matumaini makubwa sana kwani nadhani CCM ilihitaji mtu wa namna ya Lowassa kuonja changamoto za upinzani ili kuboresha namna CCM inavyowatizama wapinzani. Na kwa kiasi kikubwa sana Lowassa ameonewa aibu na vyombo mbalimbali kwa sababu ya historia na heshima yake ndani ya CCM kwani angeweza kuwa kama Mbowe hivi sasa.

Na kwa wapinzani wote waliorudi na wanaoenda CCM na wanapewa naafasi za kuamua nadhani kama wataamua watafanikisha hili kwani wameliona na wanalijua. Na kama hawalijui basi kupitia andiko hili wajue na hivyo waamue. Binafsi nadhani Watanzania tunahitaji kina Lowassa wengi zaidi ndani ya CCM kuliko kina Lipumba wengi ndani ya upinzani. Wasalaam.
 
Wakimbizi wa Burundi hurudi Nyumbani kwao kutoka Kigoma hali ikirejea Tulivu

Ndugu Lowassa alikuwa Mkimbizi wa Kisiasa pale Ufipa lakin kwa kukurupuka kwao 'Mkimbizi' wa Kisasa akapewa fursa ya Kuwa ndio Rais Mtarajiwa
 
mawazo finyu katiba upuinzani ndio waliyoikataa bunge la katiba walikuwa wanatoka nje kama taifa hatuwez kukalia jambo moja tu
 
Umenena vema kiasi chake.
Swali chonganishi
Ikitokea Lowassa akapewa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM vipi wapinzani wamuunge mkono ili aje kuwainua?
Wapinzani wasimuunge mkono kwa sababu anawajua nje ndani?
Ukiyajibu hayo nitakuja ten
 
Watu wenye roho ngumu,za kujitoa kama Mandela,hawapo siku hizi.
Kwa maumivu wanayopata wapinzani,vipigo,kufungwa,mauaji,inabidi uwe na akili kama kichaa kubaki upinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema kiasi chake.
Swali chonganishi
Ikitokea Lowassa akapewa nafasi ya kugombea urais kupitia CCM vipi wapinzani wamuunge mkono ili aje kuwainua?
Wapinzani wasimuunge mkono kwa sababu anawajua nje ndani?
Ukiyajibu hayo nitakuja ten
Akipewa hiyo naafasi lazima atakua na ilani ambayo ina agenda za chama. Kwa mfano anaweza akasema akichagulia atabadili katiba. Katika hili wapinzani wanaweza wakamuunga mkono na hakutakua na tatizo lolote. Ila akisema ataendeleza pale alipoishia JPM kuhusu kutoruhusu wasichana wenye ujauzito kutoendelea na masomo. Hapa wapinzani wanaweza kupinga na kunadi sera yao mbadala ya kuruhusu waendelee au kubuni sera tofauti itakayounda mfumo mbadala kuruhuau waendelee na masomo wakishajifingua. Na katika hili pia hakutakua na shida yoyote. Natumaini nimejibu swali lako.
 
Back
Top Bottom