Mtamuua Magufuli.
Anadhani baada ya Tamko lake la Jana, basi kila kitu kitakuwa shwari na watu watanyamaza. Ndio kwanza kawasha moto.
Halafu Magufuli anadai kuuza nyumba zote za umma, Dar Es Salaam. Ni lini Bunge lilikaa na kukubaliana azimio hilo la kuuza nyumba za umma?
Na ni kampuni zipi zimepata tenda ya Auction a.k.a kuendesha mnada? Na lini tenda imetangazwa?
Haya ni maamuzi ya Kichwani au Baraza la Mawaziri? Au ni mzuka wa kulazimisha matukio badala ya kubadili mfumo kisheria kikanuni na kitaratibu za nchi?