chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Edward Lowassa amesema kwa sasa CHADEMA wameachana na siasa za kiharakati na sasa wamegraduate na kuwa chama cha siasa, amesema wana harakati huwa wanagomea mambo, kufanya maandamano na kuzuia serikali isifanye kazi yake, lakini sasa wamekuwa chama cha siasa ambayo vision yake ni kukamata dola
Nionavyo
ujue kwa kipindi cha miaka ya Kikwete CHADEMA imekuwa kubwa kweli na hali ingeendelea kama kwenye kipindi cha Kikwete nadhani CHADEMA wangekuwa wanafanya aina ya siasa aliyoitaka Lowassa hapa ila kwa huyu aliyeingia madarakani sasa hivi naona yeye ndio analazimisha CHADEMA wawe wana harakati kwa kuturudish tena nyuma kama jenerali ulimwengu alivyosema
Maandamano kwa siasa za Afrika bana ni muhimu, hasa kwa serikali na vyama tawala ambavyo havisikilizi upinzani kama Kenya walikuwa wanataka tume mpya lakini serikali ikabana jamaa wakaingia mtaani, serikali ikaja kwenye majadiliano