Lowassa azua mapya

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
WAZIRI Mkuu wa zamani aliyejiuzulu baada ya kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, Edward Lowassa, amezua mambo mengine mapya matatu, baada ya tukio la kutangaza nia ya kuwania urais, Jumamosi iliyopita.

Miongoni mwa mambo hayo ni gharama kubwa za kuandaa mkutano huo zikihusisha za kusafirisha na kuwalipia mamia ya wageni malazi na chakula, na hapo hapo, kwenda kinyume cha ahadi yake kwamba angezungumzia kwa undani kashfa ya Richmdon dhidi yake. Vile vile, Lowassa amezua mjadala kuhusu nini hasa kilimsukuma kutumia fedha nyingi zinazokadiriwa kufikia shilingi bilioni moja kwa ajili ya kutangaza nia tu.

Kukwepa hoja ya Richmond Kinyume cha matarajio ya wengi, Mbunge huyo wa Monduli (CCM), Jumamosi iliyopita "alikwepa" kuzungumzia sakata la ufisadi wa kampuni hiyo ya kufua umeme ya Richmond wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia ya kugombea urais uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Habari zilizopatikana kutoka kambi ya mgombea huyo zinadai kuwa Lowassaalilazimika kuacha kuzungumzia suala la Richmond tofauti na kauli aliyoitoa awali katika mkutano wake na wahariri wa vyombo kadhaa vya habari mjini Dodoma baada ya kushauriwa na watuwake wa karibu.

Taarifa hizo zinabainisha kuwa washauri wake walimweleza kuwa kuzungumzia Richmond ilikuwa sawa "kutia kidonda chumvi" kwani lingewagusa watu ambao ndiyo wanaotarajiwa kushiriki mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya chama chake cha CCM."Ndiyo ni kweli Mzee alishauriwa aachane na "ishu" ya Richmond asubuhi ya siku ya mkutano huo baada ya kushauriwa na "kamati yake ya ufundi" iliyosheheni wataalamu wa Sayansi ya Siasa kuwa suala hilo litawagusa viongozi wengine ambao niwashiriki katika vikao vya uamuzi vya CCM," kilieleza chanzo chetu.

Mara kwa mara Lowassa amekaririwa akieleza kuwa hakuhusika na ufisadi wa kampuni hiyo ya Richmond na kujiuzulu kwake kulitokana na imani yake aliyonayo kwa chama chake na serikali na alikubali kujiuzulu ili kunusuru taasisi hizo.


Chanzo: Raia Mwema
 
Je? Waweza mtuumu mwalimu wako wa darasa / na wewe u ngali ndani ya darasa hilo???
Common sense matters!!!
 
Ulipiga hesabu za hizo hela au ni kutaka kumchafua Edo..!? acha unafiki wewe na wenzako, au hao wengine ni wasafi? Lowassa ndiye habari ya mjini kwa sasa kataeni mkubali..!!
 
wengi tulitaka kuskia kuhusu kashfa ya richmond tujue mchaw ni nani na mwema ni nani?
 
Ulipiga hesabu za hizo hela au ni kutaka kumchafua Edo..!? acha unafiki wewe na wenzako, au hao wengine ni wasafi? Lowassa ndiye habari ya mjini kwa sasa kataeni mkubali..!!

Mkuu hyo habari sijatunga.....ni gazeti limeripoti hayo.
 
Moja ya Disadvantage ya Lugha ya kiswahili ni kwamba ina Maneno meeeengi lakini UKITAFUTA CHA MAANA hata hakijazi kijiko cha chai. Tz tunaitumia hii lugha kupiga Majungu na Fitina tu.
 
Moja ya Disadvantage ya Lugha ya kiswahili ni kwamba ina Maneno meeeengi lakini UKITAFUTA CHA MAANA hata hakijazi kijiko cha chai. Tz tunaitumia hii lugha kupiga Majungu na Fitina tu.

Wameandika waandishi wa gazeti la Raia Mwema mkuu
 
Huyu mtu sitaki tena kumjadili maana napoteza muda wangu bure kumjadili mjinga ambae hata kama atapitishwa kwa upande wangu bado ataendelea kuwa hopeless tu.
 
Watanzania tunasikitisha sana, yaani cha kushangaza hadi baadhi ya makamanda wa Chadema kule Arusha wanamshabikia Lowassa, upinzani uko wapi sasa hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…