Kwa kwenda ofisi za serikali kushitaki mjue siku zote mtapotezewa ,wala hamna haja ya kuripoti makao makuu ya Chama ,ila kitu kimoja ni just kuweka taarifa ya kinachojiri huko ,polisi na hata makao makuu ya chama '
Iwapo mna uhakika kuwa siku ni yenu ya kufanya mkutano hapo na stakabazi zote mnazo basi kinachotakiwa ni kwa nyinyi nanyi kufunga vyombo vyenu ,tena mjizatiti kikwelikweli kwa liwalo na liwe ,mambo ya kwenda kushitaki yamepitwa na wakati ,ifike wakati wanaoshitaki wawe miccm na sio upinzani na wakati ni huu.Haki yenu haitaletwa na kupewa ndani ya sinia na sahani ,inatakiwa muilinde na muichukue kwa hali yeyote ile. Mlete habari kuwa mumefanikiwa kuilinda na sio mmekimbilia vyombo vya serikali,serikali ambayo ni miccm ,mpo ,kazeni buti mpaka kieleweke.