Lowassa aungana na Maaskofu kutaka yafanyike maombi ya kitaifa kuombea mvua.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487


WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ameungana na maaskofu wa Kanisa Katoliki kutaka yafanyike maombi ya kuliepusha Taifa na baa la njaa.
Hiyo ni baada ya kuwapo ukame wa muda mrefu nchini uliosababisha mazao mengi kukauka.

Lowassa ametoa kauli hiyo siku moja baada ya maaskofu wa kanisa hilo kupitia Mwenyekiti wa Baraza lao, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, kutaka iongezwe kasi ya maombi kwa kuwa baadhi ya maeneo nchini tayari yana uhaba wa chakula.

Alikuwa akitoa salamu zake katika Kanisa la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Mjini Bukoba ambako alikuwa miongoni mwa waumini kanisa hilo waliohudhuria misa ya kwanza.

Lowassa alisema si jambo la siri tena kuwa Taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la njaa.

Aliwashauri viongozi wa dini kwamba maombi ya kuliepusha taifa na baa la njaa na ukame viwe miongoni mwa vipaumbele vyao na kuwataka waumini wa madhehebu yote kuungana na viongozi wao kuliombea taifa.

“Nawaomba viongozi wa dini ikiwezekana msimamishe hata mambo mengine na kutoa kipaumbele cha kuliombea taifa letu.

“Wote mnajua hali ya chakula siyo nzuri katika maeneo mengi ya nchi, sisi hatutachoka kuwasaidia wananchi,’’ alisema Lowassa.

Pamoja na kuwapo matamko mbalimbali ya viongozi wa Serikali yanayokatisha tamaa wananchi, Lowassa alisema wao hawataacha kuwasaidia wananchi wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali.

Aliwataka viongozi wa dini kufanya hivyo pia.

Alisema yuko Bukoba kuwapa pole kwa ukame pamoja na janga la tetemeko ingawa alifika mkoani humo mwaka jana na kuwasilisha mchango wa mifuko 400 ya saruji kwenye kamati ya maafa ya mkoa.

Source: Mtanzania
 
Back
Top Bottom