Lowassa amtoa kafara Pinda

Lowassa amtoa kafara Pinda

mr traders

Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
38
Reaction score
15
RIPOTI ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka 2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam, imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.

Pinda anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Kutokana na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa chini ya kiwango.

Duru za siasa kutoka ndani ya Bunge zinasema kuwa tayari kuna baadhi ya wabunge bila kujali itikadi zao, wameunganisha nguvu kutaka kumsulubu Waziri Pinda katika mkutano ujao wa Bunge kupitia hoja binafsi au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.

Mmoja wa mawaziri waandamizi wa serikali ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema: "Pinda anastahili kubeba mzigo, kwani baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?

"Kwa uzembe huu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hakuwawajibisha waliojenga kinyume na utaratibu hadi Watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika." Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema (TLP) alimshangaa Waziri Pinda kwa kushindwa kuchukua hatua zilizopendekezwa na tume ya Lowassa kwani ilipendekeza baadhi ya majengo yabomolewe na wahusika wachukuliwe hatua.

Alisema athari ya ukimya huo ni kuendelea kuangamia kwa Watanzania kunako sababishwa na uzembe wa viongozi wa serikali. "Hili tatizo la kushindwa kuchukua uamuzi mgumu litaendelea kutugharimu kila siku, yale maghorofa yaliyotakiwa kubomolewa kipindi kile hayajaguswa na hayataguswa kwa sababu ya kubebana, hili hatuwezi kulinyamazia, lazima tukawashe moto bungeni," alisema Mrema.

Alisema Watanzania hawapo tayari kuletewa danganya toto ya tume nyingine ikalete majibu ambayo tayari yako mezani kwa Pinda.Mbunge wa CCM aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata watendaji wa Manispaa ya Ilala hakitoshi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ataendelea kubaki ofisini.

Mrema ambaye amepata kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa nyakati tofauti, alisisitiza kuwa Waziri Tibaijuka anapaswa aige mfano wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Lowassa walioamua kuachia ngazi kutokana na uzembe wa watendaji wao.

"Kwa wenzetu leo inapotokea boti ikazama kwa uzembe na kupoteza maisha ya watu watatu waziri mwenye dhamana anawajibika, iweje sisi leo tuwachekee mawaziri wetu?" alihoji mbunge huyo. Mbunge wa kuteuliwa na rais, James Mbatia, ameapa kuwasha moto katika Bunge lijalo hadi kieleweke.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema lazima Waziri Mkuu atoe majibu ya msingi kwa Watanzania kwanini hakutekeleza maazimio ya tume ya Lowassa.
Alienda mbali na kuhoji utendaji wa kitengo cha maafa cha Waziri Mkuu kwani kimekuwa kikishughulika kutoa vyakula vya misaada kwenye maafa badala ya kudhibiti yasitokee.

"Tangu tume zianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua? Kuanzia tume ya MV Bukoba hadi tume ya matokeo ya kidato cha nne, Watanzania tumechoka kuneemesha mifuko ya wajumbe wa tume na kufilisi rasilimali zetu, hivyo Pinda, Tibaijuka lazima wajiuzulu," alisema.

Wakati wabunge hao wakitaka Pinda na Tibaijuka waachie ngazi, habari zaidi ndani ya serikali zinasema kuwa ripoti ya Tume ya Lowassa haikufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yaliyopendekezwa kubomolewa, yanawahusu viongozi wa juu serikalini.

"Ile ripoti iliwasilishwa wakati Lowassa bado yuko madarakani. Alishindwa kuifanyia kazi na haiwezi kufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yanawahusu viongozi au yanamilikiwa na watu wa karibu wa viongozi, na ndio wachangiaji wakubwa wa fedha wakati wa kampeni," kilisema chanzo chetu cha habari.

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09, Pinda alizungumzia jinsi Tume ya Lowassa ilivyofanya kazi katika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam. Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume na taratibu za ujenzi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi. Lowassa aliunda tume baada ya jengo la hoteli ya Chang'ombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa ilibaini pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.

NHC yatoa kauli

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesema kuwa mbia wao alikuwa na vibali vya mamlaka zinazohusika kusimamia ujenzi wa majengo makubwa vya kumruhusu kuongeza ghorofa 16 kutoka kumi za awali.

Kauli hiyo inakuja kukiwepo na mvutano kutoka mamlaka mbalimbali ikiwemo Manispaa ya Ilala kwamba mbia wao huyo ambaye ni M/s Ladha Construction alipewa kibali cha kujenga ghorofa kumi, lakini cha kushangaza aliongeza nyingine sita bila taarifa na hivyo kusadikiwa kuwa huenda ndiyo chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Nehemiah Mchechu akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa, alisema Agosti 22 mwaka jana mbia wao huyo aliwataarifu kuwa ameshapata vibali kutoka mamlaka husika, na kwamba angependa aingie nao mkataba mdogo kutambua ongezeko la ghorofa hizo na mabadiliko ya tarehe ya kumaliza mradi.

"Shirika lilimjibu kuwa hakuna pingamizi kama mbia ataleta nakala ya vibali kutoka mamlaka husika kwa ajili ya kumbukumbu za shirika na pia ili kufikia hatua za maamuzi ya ndani na mawasiliano yote hayo yapo kwenye rekodi zetu na endapo mamlaka husika itazihitaji tuzazipatia," alisema.

Kutokana na hali hiyo, aliutaka umma kutoliingiza shirika hilo katika sakata hilo kwa madai kuwa zipo taasisi na vyombo vinavyokasimiwa mamlaka ya kusimamia ubora wa ujenzi wa nyumba nchini, na NHC nayo husimamiwa na taasisi na vyombo hivyo.

Source: Tanzania Daima
 
Huyu Fisadi Lowassa nahangaika jamani.....!!
Lowassa ni fisadi tu .....aliyafanya yale kama binadamu tu sio kama mtu makini, msafi!!
 
Lowassa alikuwa mtendaji mzuri enzi zake, tatizo watu wanakomalia ufisadi ufisadi, hawaangalii utendaji wake wakati akiwa waziri mkuu. Kamwe siwezi kuulinganisha utendaji wa Pinda na Lowassa.
 
pinda ana matatizo, ni mzembe...wakifanikiwa kumpiga chini itakuwa fundisho tosha
 
Lowassa alikuwa mtendaji mzuri enzi zake, tatizo watu wanakomalia ufisadi ufisadi, hawaangalii utendaji wake wakati akiwa waziri mkuu. Kamwe siwezi kuulinganisha utendaji wa Pinda na Lowassa.

kaka nakubaliana na wewe. Lowasa alikuwa ni mtendaji mzuri na mzalendo. kama aliweza kuwajibika kwa ile kashfa ya richmond, ilikuwa jukumu ya szerikali ya dhaifu kuthibitisha kama alikuwa guilt au la. kwa nimuonavyo bado ni kiongozi wa kutenda nasio wa maneno na kulialia kama fisadi silent Pinda.

Kama pinda anachukua hata 280,000 kama posho kwa jairo, wafikiri kubwa zinaendaje? owasa ndio ana miradi mingi na inampatia fedha, kama sio halali sijui kini ni mtu wa kuc hakarika sana na mwenye uwezo wa kukabiliana na mambo. Baada ya sokoine ni yeye lowasa aliyethubutu kuwa mkali na mwenye kuthubutu kukemea na akasimamia kauli yake mpaka akawin. Pinda ni kama kivuli na ni mnafiki mno.

Hana dhamira ya huruma na roho yake imejawa na chuki na usaliti kama anavyoonekana usoni. siyo mtu wa maamuzi bali wa kusema tutaangalizi jinsi gani ya kufanya, tupeane muda, tutachunguza, sina la kusema, tunafanya tathmini mara mchakato na mengine yasiyo na majibu. Lowasa ni jembe na siyo mwenye husda kama huyu dhaifu na waziri wake mkuu.
 
huyu si yule bwana nanii hiii ndio anaendeleza mipango yake. Kinachonipa shida hapa ni kwamba amejaribu kuipiga vita kilimo kwanza ameshindwa, amejaribu kupiga vita kila kitu ameonesha kushindwa sasa amehamia kwenye hili. swali langu kwake ni je! haoni kwamba watanzania sio wale wa zamani wanamjua yeye na mipango yake na sasa niwakati wake wa kutambua kwamba hana lolote na akalale huko kwao. we bwana nani hii ni mtu mzima bwana usijiaibishe bwana umeshindwa kila kitu
 
Lowasa ????, watz tujifunze kutosahau mwaka 2008 fisadi wa richmondi leo shujaa. Makampuni yote anayomiliki hamuoni. He is multibilionia, ok, kuhusu jengo ni makosa makubwa kumlaumu pinda kwa sababu ana nyombo mfano nhc ambao ni mbia wa hilo jengo. Hili ni shirika la umma inakuwaje lijenge jengo below standards?. Kwamba eti mbia mwenzake alipaswa kujua ni uwongo kwa vile huwezi kuwa mbia na hujui chochote , mchechu wajibika afuate tibaijuka.
 
Huyu Fisadi Lowassa nahangaika jamani.....!!
Lowassa ni fisadi tu .....aliyafanya yale kama binadamu tu sio kama mtu makini, msafi!!
Lol yaani kuna watu wakiona tu lowassa wanatokwa na povu,pamoja na mapungufu aliyonayo kama binadamu lkn kwa hili alijitahid kutaka kujua ukubwa wa tatizo,sioni hoja ya kumpinga kwa hili zaidi ya kuungana naye na watz wengine kubaini ukweli wa matatizo,kwa sasa speed ya ujenzi wa maghorofa si dar peke yake hata mikoani kwa sasa ujenzi wa maghorofa ni mkubwa,hakuna anayefuatilia kujua kama ubora na taratibu za ujenzi unanzingatiwa,serikali iachane na kazi za zima moto,ituletee tume ya lowassa tuone walichobaini kabla ya kuunda tume nyingine
nawasilisha
 
Wana JF heshima kwenu !!

Ni vyema tuachane na mambo ya mitandao na ushabiki wa kisiasa tukajadili hili saga la ghorofa kuporomoka kwa mapana yake;
Mie binafsi simkubali Lowassa kivile, lakini ukweli unabaki pale pale kwa swala la kiutendaji huwezi kumlinganisha na Mizengwe Iliyopinda kwani ni sawa na kulinganisha usiku na mchana.

Kinacho nisikitisha ni pale wachangiaji wengi wanapoishia kusoma heading na kuanza kumshambulia Lowassa hata kabla hawajasoma habari yenyewe; Kwa mfano "huyu Lowassa kesha anza, nani asiye mjua na Richmond yake" hiyo ni mifano tu ya kuwa hao wachangiaji hawajasoma content bali wanaongozwa na mihemko yao. Nimesoma hiyo habari zaidi ya mara mbili hakuna sehemu ambayo Lowassa amenukuliwa akitoa kauli yake, kilicho ongelewa hapa ni report ya tume yake aliyo iunda akiwa waziri mkuu.

Ni dhahiri wachangiaji walio wengi wameshindwa kutofautisha Report yaWaziri mkuu kuhusiana na kuporomoka kwa magorofa na Lowassa. Wadau tunahoji kwa nini Mizengo Pinda ameyapotezea mapendekezo yaliyotolewa na tume iliyo undwa na waziri mkuu ?

Pro-Pinda mtahangaika sana kumuokoa mtoto wa mkulima kwenye hili saga, lakini kwa taarifa yenu ni vyema mkatumia hizo nguvu za kumtetea huyo mnafiki kufanya kazi zingine za maana kwani hamuwezi muokoa, Mizengo Pinda ndiye mtu wa kwanza atakaye wajibika katika hili akifuatiwa na Prof. Tibaijuka.
 
Pinda nae aende tuu maana amekuwa business as usual kwa vitu vingi tofauti na matarajio yetu!
Tibaijuka nae aende akaanze maisha mapya na ule Mlungula aliopewa kusimamia utekaji wa mji wa Kigamboni kwa mwekezani na kuongeaza eneo daily bila taarifa
 
Lol yaani kuna watu wakiona tu lowassa wanatokwa na povu,pamoja na mapungufu aliyonayo kama binadamu lkn kwa hili alijitahid kutaka kujua ukubwa wa tatizo,sioni hoja ya kumpinga kwa hili zaidi ya kuungana naye na watz wengine kubaini ukweli wa matatizo,kwa sasa speed ya ujenzi wa maghorofa si dar peke yake hata mikoani kwa sasa ujenzi wa maghorofa ni mkubwa,hakuna anayefuatilia kujua kama ubora na taratibu za ujenzi unanzingatiwa,serikali iachane na kazi za zima moto,ituletee tume ya lowassa tuone walichobaini kabla ya kuunda tume nyingine
nawasilisha

Lowassa Fisadi tu..
 
Lowassa ni jembe hasa hakuna unayeweza kumlinganisha nae . Hata wafanyakazi wote serikalini wanajua hilo na wanamwogopopa saana . Alikuwa hacheki na mtu.
 
Sioni swala la kumshambulia Lowasa, hpa kinacho zungumziwa ni swala la uwajibikaji na sio Lowasa. Kikubwa hapa ni swala la kupuuzia report ya Tume ya Lowasa baada ya kuanguka kwa jengo na kuua. Acheni ushabiki wa kijinga.
 
Wana JF,
Nimegundua kuwa watetezi wa wananchi pasipo kificho ni wanasiasa wa vyama vya upinzani. Ebu fuatilia hapo nukuu hizi:

Duru za siasa kutoka ndani ya Bunge zinasema kuwa tayari kuna baadhi ya wabunge bila kujali itikadi zao, wameunganisha nguvu kutaka kumsulubu Waziri Pinda katika mkutano ujao wa Bunge kupitia hoja binafsi au maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.

Mmoja wa mawaziri waandamizi wa serikali ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema:"Pinda anastahili kubeba mzigo, kwani baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?

"Kwa uzembe huu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hakuwawajibisha waliojenga kinyume na utaratibu hadi Watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika."
Mbunge wa Vunjo Augustino Mrema (TLP) alimshangaa Waziri Pinda kwa kushindwa kuchukua hatua zilizopendekezwa na tume ya Lowassa kwani ilipendekeza baadhi ya majengo yabomolewe na wahusika wachukuliwe hatua.

Alisema athari ya ukimya huo ni kuendelea kuangamia kwa Watanzania kunako sababishwa na uzembe wa viongozi wa serikali. "Hili tatizo la kushindwa kuchukua uamuzi mgumu litaendelea kutugharimu kila siku, yale maghorofa yaliyotakiwa kubomolewa kipindi kile hayajaguswa na hayataguswa kwa sababu ya kubebana, hili hatuwezi kulinyamazia, lazima tukawashe moto bungeni,"
alisema Mrema.

"Kwa wenzetu leo inapotokea boti ikazama kwa uzembe na kupoteza maisha ya watu watatu waziri mwenye dhamana anawajibika, iweje sisi leo tuwachekee mawaziri wetu?" alihoji mbunge huyo.
Mbunge wa kuteuliwa na rais, James Mbatia, ameapa kuwasha moto katika Bunge lijalo hadi kieleweke.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema lazima Waziri Mkuu atoe majibu ya msingi kwa Watanzania kwanini hakutekeleza maazimio ya tume ya Lowassa.
Alienda mbali na kuhoji utendaji wa kitengo cha maafa cha Waziri Mkuu kwani kimekuwa kikishughulika kutoa vyakula vya misaada kwenye maafa badala ya kudhibiti yasitokee.

"Tangu tume zianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua? Kuanzia tume ya MV Bukoba hadi tume ya matokeo ya kidato cha nne, Watanzania tumechoka kuneemesha mifuko ya wajumbe wa tume na kufilisi rasilimali zetu, hivyo Pinda, Tibaijuka lazima wajiuzulu," alisema.

Wakati wabunge hao wakitaka Pinda na Tibaijuka waachie ngazi, habari zaidi ndani ya serikali zinasema kuwa ripoti ya Tume ya Lowassa haikufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yaliyopendekezwa kubomolewa, yanawahusu viongozi wa juu serikalini.

"Ile ripoti iliwasilishwa wakati Lowassa bado yuko madarakani. Alishindwa kuifanyia kazi na haiwezi kufanyiwa kazi kwani baadhi ya majengo yanawahusu viongozi au yanamilikiwa na watu wa karibu wa viongozi, na ndio wachangiaji wakubwa wa fedha wakati wa kampeni,"
kilisema chanzo chetu cha habari.

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwa mwaka 2008/09, Pinda alizungumzia jinsi Tume ya Lowassa ilivyofanya kazi katika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam.Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100 jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume na taratibu za ujenzi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Lowassa, kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka za ujenzi. Lowassa aliunda tume baada ya jengo la hoteli ya Chang'ombe Village Inn, Keko, Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa ilibaini pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi huku mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamo wahandisi wa manispaa husika.

Source: Tanzania Daima
 
Hivi nyie watu mbona wepesi kusahau. Yaan Shetani akianza leo kugawa pesa na kupeleka zawadi kwa wagonjwa ndo tuseme huyu ni Mungu? Kinachobadilika ni muda tu Lowasa anabaki ni yuleyule: Mwizi, fisadi, jangili, mchonganishi, mnafiki, mtoa rushwa makanisan na miskitin, mhujumu uchumi. Kama kuna m2 atamsafisha basi kuna posho si bure. Matatizo ya umeme na kuyumba kwa uchumi "Prevailing cause" ni Rich wa Monduli RICHMOND chin ya uangaliz wa Lowasa. Yan hata akitaka kujiunga chadema akataliwe. KWA UJUMLA CCM HAKUNA MWENYE NAFUU. TUBADILI MFUMO TU
 
Tatizo ni pale ambapo huyu bwana nanihii anashindwa kujisahihisha mwenyewe na kuanza kumnyooshea vidole Pinda. Kwanza lazima tuone kwamba hatua zote alizochukua waziri mkuu wa kipindi hiko, jengo lilipo anguka changombe ndizo ambazo zimechukuliwa hapa. moja wapo kubwa ikiwa ni kufikishwa mahakamani kwa wahusika. mnataka pinda afanye nini? tatizo letu watanzania ni kubabatizwa na mikumbo hasa na watu wenye fedha kama huyu bwana. pamoja na hilo hapa kuna National Housing (NHC) kuna CRB, pia ERB zote hizo hamzioni? lakini zaidi sana kuna wizara ya ardhi. yani wote hao hawaonekani mpaka pinda. jamani jamani nyie mmetumwa na mna lenu jambo hapa. namnajua kuwa mmeshashindwa kabisa kwani hoja yenu haina mashiko
 
Back
Top Bottom