Waumini wa KKKT usharika wa Monduli Mjini jana walipigwa na butwaa baada ya harambee waliyokuwa wakiisubiri kwa hamu iongozwe na mbunge wa Monduli ndugu Edward Lowassa kwa ajili ya kumalizia jengo la hostel kugonga mwamba baada ya mbunge huyo kutotokea kama alivyoahidi. Awali mbunge huyo aliahidi angekuja na marafiki zake ambao alisema wana uwezo mkubwa wa kifedha hivyo waumini watarajie kupata fedha za kutosha.Lakini katika hali isiyotarajiwa waumini waliambulia patupu badaa ya Lowassa kutoonekana katika ibada hiyo ya mwaka mpya.
WAKATI HUOHUO
Wakazi wa Monduli waliokuwa wanatarajia kwenda nyumbani kwa mbunge huyo jana kwa ajili ya sherehe za mwaka ambazo wamezoea kufanyiwa kila tarehe moja ya mwezi wa kwanza nao waliambulia patupu baada ya kupewa habari kwamba hakuna chochote mwaka huu nyumbani kwa mbunge wao Ngarash. Kila mwaka wakazi wa Monduli kutoka kila kona hufika nyumbani kwa mbunge wao wengine wakitokea maeneo ya mbali kwa malori kwa ajili ya sherehe hizo za mwaka lakini sasa wapo katika mshangao mkubwa baada ya sherehe kuota mbawa.