VIVA ROMA VIVA
#nana nana nanana!!
(Tongwe records baby!!)
Verse 1
Nimeshapigwa sana mkwara na jumbe za
vitisho/ Ila siamini huu msafara ni vibaraka wa Mrisho/
Si tulianza sawa vita kuitetea ikulu/
Leo umeisaliti UKAWA kwenye sherehe za
uhuru/
Uhuru ukwapi mnasherekea uhuru??/
Uhuru wa kutowafilisi viongozi wakijiuzuru/ Na wanaokufa masikini wanangu wa
Bulyankulu/
Mungu aliwapa madini mnambinafsisha
mkaburu/
Bungeni sioni kinachoendelea/
Naona wasomi tu wakisutana umbea/ Wengine walishikwa ugoni na picha zilienea/
Hamuwaoni jimboni halafu bado mnawalea/
Mambo ya **** spika anabadili mada/
Akiona chama tawala amedhalilishwa kada/
Spika wa bunge aona analinda watu wa chama
chake/ Na bunge ni la watu wote sio chombo cha
watu
wachache/
Safari ya raisi eti tume inaundiwa tume/
Wakati Mwananyamala wanatibu TEZI DUME!!!/
KADI ya chama nachana nyongea ganja navuta/ Nikamateni si mlimshindwa TIBAIJUKA/
LETA DIFENDAAAA
LETA WAJEDAAAAA
LETA WAGAMBO ROMA nimejitoa sadaka/
Na mkitaka kuniua hakikisha sifii hapa /
nichinjeni mkanitupe kwenye daraja la Mkapa./ MAZAFA*** Walafi wa madaraka/
Hata NYERERE GADAFFI si walikufa kwa kwa
mashaka/
Sasa hakuna kiongozi msafi.. je nani mwenye
mamlaka/
Anitajie mtoto wa raisi anayesoma shule ya kata!!/
VIVA ROMA VIVA...
VIVA ROMA VIVAAA