Damu ya Tanzania mikononi mwa CCM (Gazeti la Rai) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Damu ya Tanzania mikononi mwa CCM (Gazeti la Rai)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa Hivi Gazeti La Rai Linafanya Uchambuzi wake kwa Chama Tawala; Very Interesting Article.

  Makala na Uchambuzi, Rai

  Na Prudence Karugendo

  [​IMG]

  WALIOKUWA marais wa Tunisia na Misri, Ben Ali na Hosin Mubaraka, ilikuwa imefikia kipindi wakawa wanajulikana kama madikteta kutokana na kukaa sana madarakani bila kufikiria kung'atuka.

  Lakini katika muda wote waliokuwa madarakani marais hao walikuwa wakiendesha chaguzi kila baada ya kipindi fulani ili ukaaji wao madarakani uonekane ni wa kidemokrasia, ila chaguzi zote walizokuwa wakiziendesha walikuwa wanahakikisha zinawafanya wao wabaki madarakani na hivyo kuufanya udikteta wao uonekane una ridhaa ya umma, ridhaa ya wananchi.


  Kwa njia hiyo watawala hao wakawa wameiteka nyara demokrasia ya nchi zao na kuanza kuitumia jinsi walivyotaka wao, kwa manufaa binafsi dhidi ya manufaa ya umma, umma ambao muda wote wa zaidi miongo mitatu umebaki ukitaabika bila kujua la kufanya, sababu kiufundi hali hiyo ya tabu na mateso, kwa umma wa Tunisia na Misri, ni kama ilikuwa ya kujitakia kutokana na kilichoonekana umma huo kutopenda kufanya mabadiliko.


  Watawala hao wa Tunisia na Misri, kwa kujinufaisha na hali hiyo waliyojitengenezea ili waonekane wangÕangÕaniwa na wananchi wa nchi zao kubaki madarakani, wakawa wanafikiria kuurithisha utawala wa nchi zao kwa watoto wao kama wafanyanyavyo wafalme. Kwa hiyo demokrasia ikatoka kwa wananchi na kuhamia kwenye familia za madikteta hao.


  Wananchi ambao tayari walishazungukwa wakiwa wamepokonywa demokrasia yao na kubaki kama mihuri tu ya kuidhinisha udikteta wapende wasipende, wakaamua kuvunja kuta za ngome za madikteta hao na kuamua kuichukua kwa nguvu ya umma demokrasia yao. Madikteta wakasalimu amri na kukubali kungÕoka madarakani. Kwa hiyo demokrasia katika nchi hizo ni lazima itarudi kwenye mkondo wake baada ya kupotea njia kwa zaidi ya miongo mitatu.


  Lakini pamoja na watawala hao kuondoka madarakani kwa njia hizo zinazoonekana ni za aibu, bado wamejitengenezea heshima. Wamekubali kutii amri mbele ya nguvu ya umma. Wamekiri ulaghai wao waliokuwa wakiutumia kuiadaa dunia kuwa wanang'ang'anizwa madarakani na wananchi wan chi zao. Sasa wameyatambua na kuyakubali matakwa halisi ya umma katika njia ambazo hazikuwa na aina yoyote ya uchakachuaji. Tuseme ule ungekuwa ni uchaguzi, kama walivyokuwa wamezoea, wangeweza kuuchakachua ili ionekane kwamba matakwa ya umma bado yanawataka waendelee kubaki madarakani.


  Heshima waliyojijengea inakuja namna hii; pamoja na ukweli kwamba umma ulishaamua kuwaondoa madarakani watawala hao, katika njia zisizowezekana kuchakachuliwa, bado Ben Ali na Hosni Mubarak walikuwa wameshikilia turufu kubwa ambazo zingeweza kuwabakisha madarakani kwa njia zozote zile. Kila mmoja wao alikuwa ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya nchi yake.


  Hivyo wangesema wabaki madarakani hata kwa kumwaga damu, mpaka sasa wangekuwa bado wako madarakani. Kwahiyo kwa uamuzi wao wa kukubali kuachia madaraka kwa shinikizo la nguvu ya umma ambayo lakini haikuwa na silaha ya aina yoyote zaidi ya umoja, wamejiwekea hazina kubwa ya heshima katika historia ya nchi zao ambayo si rahisi kuisha kwa karne nyingi zijazo.


  Ukweli huo unathibitishwa na nguvu za vyombo vya dola vilizonazo vya nchi zile ambazo watawala wale ndio waliokuwa waamiri wake wakuu. Tuchukulie Misri, kwa mfano, kama Mubarak angesema hatoki madarakani bila kujali ni damu kiasi gani ingemwagika, hali ingekuwaje mpaka sasa? Ni wazi kwamba utitiri wa watu ungeishateketea na bado yeye angekuwa yuko madarakani. Lakini hakutaka kufanya hivyo, akaheshimu nguvu ya umma na kuamua kuvikimbia vyombo vya dola ili vibaki kwa manufaa ya nchi na wananchi.
  [​IMG]

  Vile vile upande wa pili nako kunaonyesha kwamba elimu ya uraia ikijengeka vizuri inaleta manufaa kwa nchi na wananchi. Bilashaka vyombo vya dola, Tunisia na Misri, vimejengwa na watu wenye elimu ya uraia inayojitosheleza. Kuanzia Usalama wa Taifa mpaka majeshi ya nchi zile walielewa kwamba wenye nchi ni wananchi, kwahiyo hapakuwepo na ulazima wa kuwaangamiza wananchi ili kuwalinda madikteta ambao wananchi hawawataki. Hivyo ni imani yangu kwamba Ben Ali na Mubarak hawakuamua wenyewe kuzikimbia nchi zao bila kushauriwa hivyo na watu wa usalama wa mataifa yao.


  Katika hatua kama hizo ndipo tunapopaswa kuelewa maana halisi ya usalama wa taifa. Sababu katika baadhi ya nchi vitengo vya usalama wa taifa vimekuwa havieleweki majukumu yake hasa pale, kitengo hicho kinapojikita zaidi katika kuhakikisha tu usalama wa watawala vikiwa kimeliacha taifa zima likichungulia shimoni. Hapa maana yake ni kwamba bora taifa zima liangamie watawala wabaki salama. Eti huo ndio usalama wa taifa!


  Yanayotokea Kazikazini mwa Afrika yameanza kuwatia kiwewe watawala madikteta wa nchi zilizo chini mwa Jangwa la Sahara kikiwemo Chama Cha Mapinduzi hapa nchini. Wakati tunawaongelea watawala waliokaa madarakani kwa miongo mitatu tumekuwa tukikisahau Chama Cha Mapinduzi ambacho kimedumu madarakani kwa miongo mitano sasa. Chama hiki, tofauti na mtawala wa Libya, Muammar Gaddafi, ambaye kwa sasa naye yuko kwenye kikaango kutokana na kukaa madarakani kwa zaidi ya miongo minne lakini akiwa nalo mkononi la kuonyesha katika kujitetea, CCM haionyeshi lolote zaidi ya propaganda za kichovu zilizopitwa na wakati baada ya kukaa madarakani kwa nusu karne!


  Hata kama yapo yanayoelezeka kama ukiukaji wa uhalali yaliyofanywa na Gaddafi dhidi ya watu wa Libya, lakini walau anaweza kusema kwamba amejitahidi kuhakikisha rasilmali za nchi, ambazo yeye amekuwa akizilinda kwa nguvu zake zote dhidi ya wadoeaji wa nje ya nchi yake, zinamnufaisha kila mwananchi. Ushahidi ni kwamba katika Libya hakuna mwananchi anayepanga kwa mwenzake. Taifa lile limehakikisha kila mwananchi anamiliki makazi yake, hiyo ni mbali na posho zinazotolewa kwa watu wasio na ajira.

  Hebu tujaribu kulinganisha ushuhuda huo na wa chama tawala hapa nchini kinachopigana kufa na kupona kwa sasa hivi kutaka kulipa makumi ya mabilioni ya shilingi kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura wakati nchi iko gizani. Kwa ufupi ni kwamba CCM haina la kuonyesha kwa watu wenye akili timamu wakakubaliana nacho kuwa kinawiana na miaka hamsini ambayo chama hicho kimekaa madarakani.


  Isipokuwa kinachoonekana ni kuongezeka kwa kila shida nchini, kuongezeka kwa umasikini wakati rasilmali za nchi zikisombwa kwenda kuwatajirisha watu wa nje. Pengo linalozidi kutanuka kati ya walionacho na wasionacho. Kupanda kwa gharama za maisha kusiko na huruma kwa wanyonge nakadhalika.


  Lakini hatahivyo hayo yote ni mambo yaliyokuwa yamedhibitiwa miaka ya mwanzo ya kujitawala kwetu, ambapo kwa upande wa Tanganyika chama cha TANU kilikuwa kimejidhatiti vilivyo kuhakikisha utu wa Mtanganyika na baadaye Mtanzania unalindwa. Vilevile kwa upande wa Zanzibar ASP nacho kikiwa kimejipanga kamili kuhakikisha Mzanzibari na baadaye Mtanzania anaona nini maana ya kujitawala.


  Lakini bahati mbaya baada ya vyama hivyo kuungana na kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikaja Kiswahili cha kwamba 'chama kimeshika hatamu'! Baada ya kunogewa na utamu wa hatamu chama hicho kikaamua kujivua gamba lake na kuyapiga teke yote yaliyokuwa yameasisiwa na TANU na ASP. CCM kikawa kimejipindua chenyewe kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa chama cha mabwenyenye.

  Hilo ni kosa kubwa ambalo chama hicho kililifanya kutokana na kulewa upweke na sasa hivi kinalijutia. Sidhani kama CCM, katika ushindani kama huu kilionao kwa sasa, kingethubutu kuwatelekeza wakulima na wafanyakazi na kuwakumbatia mabwenyeye peke yao. Hilo ni kosa la kiufundi lililotokana na kujiona chenyewe ndicho kila kitu.


  Siasa, kama mchezo wa mpira wa miguu, adhabu inatolewa pale kosa lilipofanyikia. Kama ni katika eneo la hatari inatolewa adhabu kali, penalty, ambayo ni kama goli la bure. Sasa hivi CCM inaona kama upinzani umepata penalty ndiyo maana inaanza kuhaha kwa propaganda na vitisho vya kila aina. Kiwewe ilichonacho CCM ni cha kwamba penalty hiyo inaweza ikazaa goli la ushindi kwa upinzani na hivyo kukiondoa chama hicho kwenye utamu wa utawala wa miaka 50.


  Sasa hivi chama kikuu cha upinzani, Chadema, kimeshika bango nchi nzima kuonyesha yalikofanyikia makosa ya CCM kuwa ni katika eneo la hatari. Badala ya CCM kuomba radhi na kujirekebisha inakuja na vitisho na madai ya kwamba Chadema inatishia amani. Madai hayo pia yanatolewa na mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, kwamba Chadema inawatia hofu wananchi. Yaani hofu waliyonayo CCM, hasa viongozi, wanailazimisha iwe hofu ya Watanzania wote!


  Ni wananchi gani wenye kuwa na hofu na Chadema halafu wajitokeze kwa wingi tunaoushuhudia kuwalaki na kuwasikiliza viongozi wa Chadema? Tena ikumbukwe kwamba mikutano ya Chadema haina burdani, usafiri wa bure wala posho kama vinavyotolewa nyakati fulanifulani kwenye mikutano ya CCM. Eti wananchi wana hofu! Hofu ya nini?


  Uwezekano wa kuvunjika kwa amani kutokana na Chadema kuendelea kuwaelewesha wananchi musitakabali wa kisiasa katika nchi yao, unaweza ukaletwa na hofu waliyonayo CCM, na si hofu ya wananchi. CCM wanaelewa makosa yao ndiyo maana wanakuwa wepesi kutaharuki wakiwa wanaelewa hukumu inayoweza kutolewa dhidi yao. Kwahiyo hofu ni lazima wawe nayo, ni hofu ya kunyangÕanywa tonge mdomoni na wala siyo hofu ya kuvunjika kwa amani.


  Lakini iwapo CCM wangekuwa na elimu ya uraia ya kutosha, wakielewa kwamba kila chama cha siasa kilichosajiliwa nchini kinayo haki ya kutawala, wasingekuwa na hofu ila wangejipanga kukabiliana na changamoto za Chadema bila woga wala mizengwe, na kupitia njia hiyo wangekuwa wameepusha kile kinachodaiwa kwamba kinaweza kutokea, umwagaji wa damu. Lakini kwa mtindo huu wa kutojiamini unaosindikizwa na woga uliopita mipaka, sielewi kama CCM watatunusuru. Ila nina imani kwamba katika hali yoyote iwayo ukweli utasimama.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Surprisingly, what a U-Turn is this.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kazi ya Bashe imeanza kumchafua JK naogopa kulipana visasi mimi maana tutajua mengi sana
   
 4. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,836
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Huo Ndio Ukweli wenyewe Ila Ukweli Hapa Kwetu Unasemwa Kwa Kulipiza Visasi in maana muda wote wa Tabu na Mateso ya Watanzania walikuwa wapi kuandika mambo Kama Haya? Naona wanatafuta huruma ya wanunuzi wa magazeti
   
 5. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  RAI ni mwana mpotevu. Amerudi nyumbani. Tumpokee.

  hii ni makala ya kudurufu na kuigawa kama njugu mahala popote Tanzania ili watu wasome wajue. lazima tukumbuke kuwa tunaishi katika ulimwengu wa taarifa. taarifa zenyewe ndiyo hizi. tuzifikishe kwa wananchi tafadhali.

  tusiishie kurusha mawe na lawama tu jamani. hii ni nchi yetu sote. wengine wanaandika wanayoandika (kama walivyokuwa wanafanya RAI zamani) si kama wanapenda, bali wanasaka mkate na karo za watoto wao.
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wamepoteza mwelekeo wameanza kuchimbana wenyewe kwa wenyewe . WENYE AKILI WAMESHAWATAMBUA JANJA YAO! Sitalipa hata senti moja kununua gazeti la fisadi RA hata liandike nini
   
 7. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Ok possibly ni kwamba rostam alinunua kampuni na sio kina Karugendo!!!??? Maana hii hata wao wakiisoma watashtuka. Nanukuu "

  Yaani kwa kauli hiyo mie naenda kunywa kiroba(Konyagi) asubuhiiiiiiiiiii, ili furaha izidi.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Tukaribishane basi huko uliko!!

  Good points aiseee
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sasa ni wakati wa kusikia mengi tu... tena mengine ya ndani zaidi....

  Lakini kwanini wapigane chini kwa chini si waje kwa public, watubu, tuwaadhibu, ndo tuwaingize kundini!!! Maana hawawezi kujiunga na kundi letu wakakti wao wana fedha za wizi lukuki!!!

  RA, EL & fiasco just come forward to TZ public.
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hizo ni hela zako au ndio zile za ufisadi wa sadaka unao ufanya ?
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu are pissed off with his money OR viroba na konyagi zao wanazoenda kujinywea at least kufurahia mpasuko mkuu tunaousubiri?
   
 12. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  wakiendelea hivi kusema ukweli na kutubu tutakuwa pamoja nao ccm wote ni magamba japo mengine bado kukomaa kama mwandishi alivyosema sie hatuna hofu bwana nyie endeleeni na hofu zenu shikaneni uchawi sie tunasonga mbele
   
 13. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  RAI! RAI! RAI! RAI! RAI!

  Katika siku ambazo Rai wamewahi kunifurahisha ni leo. You know what? Rostam Azizi tayari kesha anza mashambulizi kwa JK na Chama chake cha Magamba? Jamani si mnajua tayari wameshamwita RA na wenzake EL na AC kuwa ni magamba na hawawataki tena? Kwanini yeye na wenzake wasianze kujibu mashambulizi???

  This is a copy never to miss! Alichoandika Prudence Karugendo ni ukweli,ukweli,ukweli mtupu kwa 100 pc.

  Naona leo Ikulu na UWT wataanza mchakato wa kufikiria kulifungua Gazeti la Rai.
   
 14. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  H. Bashe in his true colours; wakati kwafaka kumalizana na R1 ambao mambo hayaivi. Ngoja tuone na kusikia mengi.
   
 15. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bashe ameanza kula kihalali mshahara wa Rostam na sasa wameamua kama vita basi ni vita Muraa!!!but asisahau yeye sio raia akituchokonoa sana tuna mrudisha Somalia under Escort
   
 16. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #16
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  akila ugali na maharage, sio tatizo nimesema kunywa kiroba unasema masanilo kafisadi sadaka. Sadaka haifisadiwi, tunatoa kwa hiari na wazee wa kanisa wanahesabu. Mtake radhi ff. Msanilo
   
 17. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Very interesting, tutaskia mengi hasa baada ya Mapacha watatu kupewa barua zao!
   
 18. k

  kiloni JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hili ni rai kweli!!!!????
  Ama kweli ukweli unaleta uhuru!!!!!!!!?????????
   
 19. c

  chitage Member

  #19
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  unexpeted submission ya RAI,good analysis
   
 20. v

  vemmy New Member

  #20
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli afadhali ndugu zangu watanzania mmeliona hilo kwa kweli CCM ndio chanzo cha matatizo yote katika jamii hali ya maisha inazidi kuwa ngumu huku mafisadi wakizidi kupeta at the expense of the local wananchi gharama za vyakula zimepanda mara dufu kwa kweli jambo la busara ni raisi aachie madaraka CHADEMA ituletee mabadiliko tumeichoka CCM japo kelele za chura hazimzuii Tembo kunywa maji lakini kwa umoja na mshikamano tunaweza kuwateketeza CCM.
   
Loading...