Lowassa ahubiri amani na upendo

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Handeni. Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameibukia katika Kanisa la KKKT wilayani Handeni mkoani Tanga, kushiriki ibada ya Krismasi na kutumia nafasi hiyo kushukuru wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Wakati Lowassa akifanya hivyo, tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo la kupiga marufuku mikutano ya walioshindwa uchaguzi, ikiwamo kushukuru kwa kuwa haina tija.
Lowassa alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na muungano wa vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF, vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, kauli hiyo ya Majaliwa ilipingwa na chama cha Chadema, ambacho katika tamko lake kilisema inaonyesha namna CCM na Serikali yake vinavyoshindwa kuelewa kwamba kuna uhusiano kati ya dhana ya demokrasia ya vyama vingi na maendeleo.
Akiwa katika kanisa hilo, Lowassa alipopewa nafasi ya kusalimia waumini, alisema kuwa yeye ni muumini mwenzao na mara kwa mara amekuwa akienda kusali hapo kila anapopata nafasi, hivyo aliomba ushirikiano wa karibu.
Lowassa aliwashukuru wale waliompa kura kwenye uchaguzi uliopita kwa nafasi ya urais na kuwataka kudumisha amani na upendo uliopo, kwani walikuwa na imani naye ndiyo maana walimpigia kura.
Pia aliomba kualikwa kwenye ufunguzi wa moja ya makanisa hayo ambayo utafanyika siku chache zijazo, akisema yeye tayari ni mwenyeji wa Handeni na atashiriki yale yote ambayo atashirikishwa.Lowassa aliwataka Watanzania kutumia amani kama silaha ya kujiletea maendeleo yao na ya taifa.
Lowassa yuko mapumzikoni na familia yake katika shamba lake la mifugo lililopo eneo la Mzeri huko Handeni, na aliwashukuru wakazi na wananchi kwa kudumisha amani baada kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Alisema wingi wa kura walizompa yeye na wagombea wa Ukawa ni kielelezo cha namna walivyokuwa na imani kubwa kwao.
Awali, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT wilayani Handeni, Lewis Shemkala aliwataka Watanzania kumrudia Mungu kwa kubadilisha maisha yao kwao kufuata yale ambayo ameagiza kwa kuwa na roho ya imani na yenye huruma.
Shemkala alisema endapo watu watafuata miongozo ya kidini kwa kukabidhi maisha yao kwa Mungu, hata mambo ya uharifu yatapungua nchini na wananchi wataishi kwa amani na utulivu kama zamani
Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa Seuta na muumini wa kanisa hilo, Ndimmyake Mwakibinga, alisema wamefarijika kusali na kiongozi huyo mkubwa katika ibada hiyo.
Katika ibada hiyo wananchi wengi walionekana kumshangaa sana Lowassa badala ya kufuatilia ibada hali iliyoonyesha kuwa alikuwa kivutio kikubwa kwa waumini wa kanisa hilo.
 
Viva lowasa kweli wewe ni mtu wa watu. Majaliwa piga marufuku lowasa kusali kanisani.
 
Rais wa mioyo ya watu Lowassa
Lumumba wakisikia hili jina wanapoteana.
 
Lowasa MABADILIKO Lowasa........... Mabadiliko LOWASA Mabadiliko.
 
JK Nyerere alizaliwa 1922
AH Mwinyi alizaliwa 1925
BW Mkapa alizaliwa 1938
JM Kikwete alizaliwa 1950
JP Magufuli alizaliwa 1959
Natabiri, next president wa TZ atakuwa aliyezaliwa kati ya 1960 na 1970.
Wazee fulani wasahau tu. Tunasonga mbele!
 
Wakati wa kuomba kura aliwaomba hao hao kanisani Tabora.....pia sio vibaya akiwashukuru hao hao kanisani Tanga
 
JK Nyerere alizaliwa 1922
AH Mwinyi alizaliwa 1925
BW Mkapa alizaliwa 1938
JM Kikwete alizaliwa 1950
JP Magufuli alizaliwa 1959
Natabiri, next president wa TZ atakuwa aliyezaliwa kati ya 1960 na 1970.
Wazee fulani wasahau tu. Tunasonga mbele!
rais ajae ni Zito kabwe makanika
 
Handeni. Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa ameibukia katika Kanisa la KKKT wilayani Handeni mkoani Tanga, kushiriki ibada ya Krismasi na kutumia nafasi hiyo kushukuru wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Wakati Lowassa akifanya hivyo, tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo la kupiga marufuku mikutano ya walioshindwa uchaguzi, ikiwamo kushukuru kwa kuwa haina tija.
Lowassa alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na muungano wa vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF, vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, kauli hiyo ya Majaliwa ilipingwa na chama cha Chadema, ambacho katika tamko lake kilisema inaonyesha namna CCM na Serikali yake vinavyoshindwa kuelewa kwamba kuna uhusiano kati ya dhana ya demokrasia ya vyama vingi na maendeleo.
Akiwa katika kanisa hilo, Lowassa alipopewa nafasi ya kusalimia waumini, alisema kuwa yeye ni muumini mwenzao na mara kwa mara amekuwa akienda kusali hapo kila anapopata nafasi, hivyo aliomba ushirikiano wa karibu.
Lowassa aliwashukuru wale waliompa kura kwenye uchaguzi uliopita kwa nafasi ya urais na kuwataka kudumisha amani na upendo uliopo, kwani walikuwa na imani naye ndiyo maana walimpigia kura.
Pia aliomba kualikwa kwenye ufunguzi wa moja ya makanisa hayo ambayo utafanyika siku chache zijazo, akisema yeye tayari ni mwenyeji wa Handeni na atashiriki yale yote ambayo atashirikishwa.Lowassa aliwataka Watanzania kutumia amani kama silaha ya kujiletea maendeleo yao na ya taifa.
Lowassa yuko mapumzikoni na familia yake katika shamba lake la mifugo lililopo eneo la Mzeri huko Handeni, na aliwashukuru wakazi na wananchi kwa kudumisha amani baada kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Alisema wingi wa kura walizompa yeye na wagombea wa Ukawa ni kielelezo cha namna walivyokuwa na imani kubwa kwao.
Awali, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT wilayani Handeni, Lewis Shemkala aliwataka Watanzania kumrudia Mungu kwa kubadilisha maisha yao kwao kufuata yale ambayo ameagiza kwa kuwa na roho ya imani na yenye huruma.
Shemkala alisema endapo watu watafuata miongozo ya kidini kwa kukabidhi maisha yao kwa Mungu, hata mambo ya uharifu yatapungua nchini na wananchi wataishi kwa amani na utulivu kama zamani
Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa Seuta na muumini wa kanisa hilo, Ndimmyake Mwakibinga, alisema wamefarijika kusali na kiongozi huyo mkubwa katika ibada hiyo.
Katika ibada hiyo wananchi wengi walionekana kumshangaa sana Lowassa badala ya kufuatilia ibada hali iliyoonyesha kuwa alikuwa kivutio kikubwa kwa waumini wa kanisa hilo.

Kumbe ni kweli alilosema Mzee Makamba kuwa Lowassa na marafiki zake walijiuzia ranchi?
 
Pia aliomba kualikwa kwenye ufunguzi wa moja ya makanisa hayo ambayo utafanyika siku chache zijazo, akisema yeye tayari ni mwenyeji wa Handeni na atashiriki yale yote ambayo atashirikishwa.

Kaona Magufuli hatanii aliposema atachukua maeneo yote ya ranchi ambayo hayatumiki ipasavyo na kuwagawia wananchi.Lowasa kaona ahamie huko aite na vyombo vya habari ajionyeshe kuwa yeye hilo shamba analitumia ili Magufuli asilichukue. Lowasa mjanja.Kaona shamba litaondoka akibaki Monduli au Dar katimka mwenyewe mbio.Chezea Magufuli.Magufuli endelea kukakamaa hivyo hivyo.
 
tehtehteh Haya Rais wenu Lowassa. Hata Yanga wana Rais. Siku moja hata vichaa watatangaza Rais wao. Lakini Rais wa Jamhuri ya Tanzania ni Dr John Pombe Magufuli kutoka Ccm. Mezeni tu hiki kidonge japo kichungu
 
Back
Top Bottom