Loan board acheni ubabaishaji lipeni hela za watu

Loan board acheni ubabaishaji lipeni hela za watu

king herode

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
370
Reaction score
572
Habari wadau wa elimu,

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa pumzi hii ninayotumia mpaka sasa. Nianze na kadhia yangu niliyoipata heslb, mwaka jana baada ya SSH kuamua kuondoa baadhi ya makato gandamizi kwny mikopo ya elimu ya juu..

Nilipoingia kwny website yao nikakuta deni ambalo nikajitutumua na kulilipa lote.nilipoenda kuchukua final statement nikakuta kuna hela kama laki 5 hv imezidi so wanatakiwa wanirudishie..

Nikawasiliana nao wanadai kuwa natakiwa niombe refund kwa kupitia website yao online afu baada ya siku 90 nitakuwa nishapata pesa yangu.

Shida yangu ndo ipo hapa nimefanya application mwezi wa 10 mwaka jana mpaka sasa ni zaidi ya siku 150+ hakuna hata dalili ya kurefund hela yangu,ukiwapigia simu wanadai system ni mpya wanafanyia kazi tuanze kulipwa ...yaan zaid ya siku 70 zimepita wanadai eti wanafanyia kazi.

Loan board achen uhuni lipen hela za watu tumemaliza madeni yenu kiroho saaf tulipeni refunds zetu..
 
Naomba namba zao namm niwapgie maana namm nina shida km yako
 
Inabid tuwaibukie siku hawa wahuni
Unatakiwa uwe na akili shida sio bodi shida ni serikali pesa hakuna.

Ingekua shida ni bodi ungeskia washafukuzwa kazi wote.. sasa watafukuzwa vipi wakati wao sio tatizo?
 
Back
Top Bottom