Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,986
Wadau wote tukutane hapa kupeana udambwi dambwi wa mechi ya leo usiku.
Kwanza tutangulize dua zetu kwa wawakirishi hawa wa Africa Mashariki.
Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Tanzania......
=================================
FT: MO Bejaia 1-0 Yanga SC
=========
KIKOSI CHA YANGA LEO.
KIKOSI:
1: Deo Dida
2: Mbuyu Twite
3: Oscar Joshua
4: Kelvin Yondani
5: Vicent Bossou
6: Thabani Kamusoko
7: Simon Msuva
8: Harouna Niyonzima
9: Donald Ngoma
10: Hamic Tambwe
11: Deus Kaseke
BENCHI:
- Ally Bathez
- Mwinyi Ngwali
- Pato Ngonyani
- Antony Matheo
- Juma Makapu
- Godfrey Mwashiu
========
Dakika 90 za mchezo wa kwanza kwa Yanga hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika zimemalizika.
MO Bejaia 1 - 0 Yanga SC
90+1′ Mwinyi Haji anaoneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa MO Bejaia
Zimeongezwa dakika 4 za nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika
86′ Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Amis Tambwe nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony
> wakati huohuo MO Bejaia wanafanya mabadiliko pia
78′ MO Bejaia wanafanya mabadiliko kwa mara nyingine tena
76′ Geofrey Mwashiuya anapoteza nafasi ya wazi kuisawazishia Yanga
72′ MO Bejaia wanafanya mabadiliko, anatoka mfungaji wa goli Yassin Salh
69′ Kipindi cha pili kinaendelea MO Bejaia bado wanaongoza kwa bao 1-0 (MO Bejaia 1-0 Yanga)
62′ Yanga sasa wanashambulia kwa nguvu…Wanajenga vizuri mashambulizi yao na timu inaonekana ina muunganiko mzuri. . Kona ya pili mfululizo Yanga wanapata inapigwa kona ile lakini walinzi wa Mo Bejaia wanaokoa. Ngoma, Ngoma anatokea mlinzi wa Bejaia anaosha mpira unarudishwa tena langoni mwa Bejaia Msuva. Msuva anawekwa chini na Hadhiri mpira ni faulo mlinzi wa Bejaia analimwa kadi ya njano. Faulo inapigwa na Mwinyi mpira unatoka nje.
Bejaia 1 – Yanga 0.
Kipindi cha pili kimeanza. Bado MO Bejaia wanaongoza, Bejaia 1 – Yanga 0.
Mpira ni mapumziko mechi ya hatua ya makundi kati ya MO Bejaia dhidi ya Yanga, MO Bejaia 1-0 yanga
45′ Zinaongezwa dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na timu kwenda mapumziko, MO Bejaia 1-0 Yanga
42′ MO Bejaia wanapata mpira wa adhabu, unaopigwa na Sufian lakini unaokolewa na mabeki wa Yanga
41′ Yanga wanapata kona fupi…Niyonzima anamuanzaia Msuva
Msuva anatumbukiza krosi kwenye lango la MO Bejaia lakini Ngoma yuko kwenye eneo la kuotea
32′ Haji Mwinyi anaingia kuchukua nafasi ya Oscar Joshua ambaye ameumia na kushindwa kuendelea na mchezo
Bejaia 1-0 Yanga
Goli la Mo Bejaia Yassin limefungwa na Yassin Salh
20′ Yassin anaiandikia MO Bejaia goli la kwanza baada ya walinzi wa Yanga kuchelewa kuondoa mpira uliokuwa unazagaa langoni mwao. MO Bejaia 1 – 0 Young Africans
14′ Deo Munishi ‘Dida’ anafanya kazi ya ziada nyingine baada ya kuokoa mchomo mkali…MO Bejaia wameanza mchezo huu kwa kasi kubwa kujaribu kupata goli la mapema! Yanga wanajibu mashambulizi kwa mahesabu zaidi ili kumiliki presha hii. MO Bejaia 0 – Yanga Afrika 0
9′ Donald Ngoma anafanyiwa madhambi na Mlinzi wa MO Bejaia. Mpira ni faulo anaenda kupiga Haruna Niyonzima. . Anarudi nyuma moja mbili taaaaatu anapiga kula lakini mpira unawababatiza safu ya ulinzi ya Bejaia. MO Bejaia 0 – 0 Yanga
Dk 5. MO Bejaia 0 – 0 Young Africans. Mpira ni goal kick unapigwa kuelekea lango la Mo Bejaia