LIVE UPDATES: Mazishi ya Muhammad Ali

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Makumi ya maelfu ya watu wamemuaga
aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.



17.00pm:Karibu katika mazishi ya Muhammad Ali. Umati mkubwa wa watu utachukua mwili wake na kuupitisha katika maeneo muhimu ya maisha
yake kabla ya kupelekwa katika maziko.

17.05pm: Msafara huo unatarajiwa kuchukua takriban saa moja na nusu

17.09:pm :Gari lililobeba mwili wa Ali bado halijaondoka katika nyumba ya ibada ya mazishi lakini watu wengi wamejipanga kando kando ya barabara kuupokea na kumuaga shujaa wao.

Mwili wa Ali bado haujawasili lakini mamia ya watu wa Loisvile wamejipanga barabarani kuweza Kushuhudia shujaa wao!


Rais Obama hatakuepo kwa sababu ya Graduation ya Mwanae Maria ambaye anahitimu high school leo lakini Rais Bill Clinton atakuepo!
82aa9ee946b448e3e5fcd2c36201ccea.jpg



Safari ya Mwisho ya Mohamed Ali imeanza Nje ya Nyumba yenye msiba kuna nguo zilizoandikwa maandishi ya Kiarabu huku makundi ya watu yakiimba jina lake "Ali" "Ali"


Hapa ndipo Mohamed ali Alipokulia
4461db022a1f7c7b5cae8e1a0d8cd0e7.jpg



Kutokana Na msemo wa Muhammad Ali’s “Float like a butterfly, sting like a bee,” Gari nyingi zina alama ya Kipepeo

b00702235e97303e93381029fba59d33.jpg

Shabiki akiwa msibani na alama ya kipepeo

Gari aina ya Cadilac XT ikiwa imepambwa na bendera ya kipepeo
6a935b81da685ce8c67e14b51fae3584.jpg


Wakazi wa Louisvile wakiwa msibani
bb61bdc635b0d009d965f5a64be699de.jpg

e36dd2a28653d72558e3ea61357242b0.jpg

1b5668c97270ab01033ca7f844106a70.jpg
f3b6d0567d3eb6c7fe3b9b406ae1d8aa.jpg
7c61f3906dc379013271434a5aed6dd7.jpg
383a77f2274c4bc6a048ec0c595c52ff.jpg

0d4ebfb88106bb724ebf137dac5e6b4d.jpg
5b50ce3448ad36eb01f9546c06f644cc.jpg




Aliyekuwa gwiji wa mchezo wa mpira wa vikapu upande wa wanaume Kareem Abdul Jabar
amemtaja Ali kuwa nduguye na rafiki mkubwa katika mahojiano na BBC.Amesema kwamba walijuana tangu walipokuwavijana.Muhammad
Ali ni mfano wa shujaa anayeishi .Amekuwa na ushawishi mkubwa katika vizazi na mashabiki
duniani akiwa mwana michezo na mwanaharakati wa haki za kibinaadamu.katika maisha yake yote amekuwa mtu wa huruma.


Kuwepo kwa maelfu ya watu katika
mazishi ya Muhhamad Ali wakiwemo viongozi kutoka mataifa tofaut duniani kunaonyesha atahrai yake duniani kama shujaa.Ali alipigana katika mataifa 12 tofauti katika kipindi chake.chote za masumbwi pamoja na kuhudu kama.mwanaharakati wa haki za kibinaadamu.



kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kuhudhuria mazishi ya Muhammad Ali licha ya kufunga safari nchi Marekani kuhudhuria kumeangaziwa na magaeti mengi ya Uturuki.


Kwa sasa msafara umefika katika eneo la Boulevard


Maelfu ya watu wamejipanga kandokando ya barabara wakirushia maua gari lililobeba mwili wa Ali.
 
kazi ya mungu haina makosa...tangulia tupo nyumayako mungu ndie Muweza wa yote
 
Na mimi pia natarajia kuwepo kwa shunghuli maalum ya kimila ya kabila la Ali
 
Back
Top Bottom