Live kutoka kuzimu!

Hivi unadhani Mshana Jr mganga basi?kasoma Kwa ma monk huko we ndio unadhani mganga
Monk ni waabudu miungu na baba wa Miungu ni Ibilisi na shetani.

Hakuna urafiki kati ya Giza na Nuru!!

Monk na YESU hawapikiki chungu kimoja.

Jina la YESU kristo wa Nazareth pekee linatosha kukulinda na wachawi ukiliamini, haliitaji msaada wa chumvi ya mawe!!

Aamen
 
Mauongo matupu haya
 
2Wafalme2:19-21

19:Watu wa mjini wakatoka wakamwambia Elisha,tazama twakusihi mahali pa mji huu ni pazuri kama bwana wangu aonavyo,lakini maji yake hayafai ,na nchi huzaa mapooza
20;Akasema nileteeni chombo kipya mtie chumvi ndani yake,wakamletea

21;Akatoka akaenda mpaka chemchem ya maji ,akatupa Ile chumvi mle ndani,akasema BWANA asema hivi nimeyaponya maji Haya,hakutoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.

Huwa unapata muda wa kusoma maandiko Kweli?Chumvi Ina historia tangu enzi na enzi
 
Maana kama am avyo Mungu alikuumba na kutoboa matundu ya pia Kwa KAZI ya kuvuta hewa safi, asingeshindwa kumuumba mtoto akiwa ametobolewa masikio kama angependa wavae hereni

Mmhhh[emoji848][emoji848][emoji848] kwahiyo wanaume wanapoenda tohara ni kosa..!! au watu wanaponyoa nywele ni kosa ?..kwamba nywele zote zimewekwa kwa makusudi....ukifa umekwangua upara huko chini,kule kuzimu utatokea na upara wako na adhabu za kutosha ?[emoji55][emoji848]

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Nimesoma na ninakiri hili ni Neno la Mungu Kutoka kwenye BIBLIA,

Nabii wa Mungu Elisha Alipewa maelekezo kutumia chumvi Ili kuiponya kisima kisizae mapooza,

Yesu pia alitumia maji na udongo kuyachanganya kumponya kipofu,

Wapi wewe Joannah Yesu akikutokea na kukwambia unyunyize maji ya chumvi ya mawe kujikinga na wachawi?

Tumia Jina la YESU pekee kukulinda na kufungua Kila vifungo, kutumia chumvi bila kuelekezwa na Yesu , chumvi hiyo hiyo inageuka uchawi,

Chunguza vizuri ndoto unazoota, lazima umeanza kufundishwa uchawi na usipoacha utakuwa mwanga kamili.

Shetani hugeuza maandiko in his favor.

Amen
 
Nimegundua wengi tuna mambo yasiyo furahisha machoni,masikion, na hata mioyon sasa tuna hofu kama sisi hatufurahishwi na mienendo yetu vipi kwa Muumba wetu..?

Ila usitujaze uoga maana mwenye dhambi ya kula papuch, mwizi, mlevi na wenye matukio kama Hitler,koni,osama,kibwetele hata wachawi na waganga wote wataadhibiwa pamoja(mimi nimejitoa nna Mungu).
Kwa hivyo ukiamua dhambi bora ujikubali sio ukutane na Iddy Amin Dada kwa utam wa serengeti lager tu....
Mambo mengine bhana yan upelekwe kuzimu kwa ajili ya punyeto c bora ule kabisa poch manyoya mpaka uwah kwa HIV
 
Tohara Mungu aliagiza waisraeli wafanye Kwa watoto wao kuonyesha tofauti Yao na mataifa mengine.

Manabii pia Mungu ameruhusu kutonyoa ikiwa ni Mnadhiri wa Mungu.

Bt Mwanaume KICHWA chake ni muhimu kinyolewe, mwanamke kuacha nywele zake kama kifuniko Cha KICHWA chake ni sawa.

Lakini kufuata mitindo ya kidunia Kwa wana wa Mungu ni DHAMBI.

Mfano Mwana wa Mungu kuvaa nguo zilizochanwa mapajani ni dhambi inayotosha kukutupa kuzimu ukifa.

Kuvaa nguo zilizochanika sehemu sehemu, au kusuka Rasta ni mitindo iliyobuniwa kuzimu.

Ni ya kuzimu kubuni mitindo hiyo ni kumfanya anayevaa nguo za kuchanika au kusuka Rasta awe kichaa. Na mapepo hayo yanaishi jalalani. Ndomana vichaa hukaa jalalani na kuwa na mwonekano wa Rasta.

Waangalie vijana wanyoa viduku, wafuga Rasta akili zao, zinaelekea kuwa vichaa kamili.

Kufuga kucha ndefu Nia ya Mapepo yaliyobuni mtindo huo ni ufanane na Misukule Ili baadae uchukuliwe msukule baadae uende Kuzimu.

Ukifuga kucha ndefu ukidhani ni urembo, ukinyoa viduku, au kusuka Rasta na unasali, ukifa, utakataliwa GETI la Mbinguni na kurudishwa kutupwa KUZIMU ya moto.

Lazima iwepo tofauti ya Wana wa Mungu na Wana wa Giza.

Haifai kufanana nao, aliyeokoka analegezaje suruali? Kulegeza suruali nia ni uwe shoga au mfiraji.

Na mashoga na wafirahi Mbinguni hawaingii.

Huo ni UKWELI. Kubali uokolewe au kataa uhukumiwe


Aamen
 
Mkuu nakuhakikishia hujui maandiko sawasawa kama ujionavyo unayajua,hivyo punguza sana kujiaminisha kuwa hupaswi kufundishwa maandiko haya,ni kosa kubwa sana kujikinai,badala ya kuokoa wengi kama unavyodhani,utapoteza wengi zaidi na yawezekana umeshawapoteza hata wengine kwa uzi wako huu kibaya zaidi na wewe unaweza kupotea pia na hii inaniumiza sana.

Wewe umetaka hapa nikujibu,lakini maswali yangu yote niliyouliza hujajibu bali kuweka maneno ya uongo unayotunga mwenyewe ukiunga na vifungu vya biblia visivyohusiana,sasa nakuambia,wewe kufanya hivyo si sawa.

Katika maandiko haya,heri kama kitu huna ufahamu nacho uwe kimya tu si kupotosha.

Naomba nianze kujibu maswali yako hapa chini post inayofuata,ndani ya majibu nitaweka maswali ya wewe kukaa kuomba na kutafakari (ikiwa hii ni desturi yako,maana sina hakika kama unatafakari kabla ya kuandika chochote na ndio maana unapata nguvu ya kuita wanadamu wenzako wana dini ya kuzimu au farisayo).
 
Umesema "ibrahimu alitokewa na malaika waliovaa miili ya wanadamu na wakashiriki chakula", hii nakubali ni kweli.
Lakini tabua malaika kwao neno roho halijasimama kama unavyolitumia wewe,na ndio maana nikakuuliza roho ni nini?,
Sasa kumbe ili roho ile chakula lazima iwe na mwili wa kula,ila hizo roho unazosema wewe za kuzimu zina mwili ni zipi hasa,maana miili hii tunakuwa tumeizika,na ukisema mtu akifa anaenda sijui kuzimu kuanza kutumikia hukumu mara moja au paradiso huo ni uongo na mafundisho yaliyojaa upotovu,maana YULE aliyefufuka,alifufuka na siku ileile ya jumapili asubuhi alimwambia mariam magdalene kuwa "usinishike maana sijaenda kwa BABA",kumbuka anasema hivyo baada ya kufa na kufufuka,sasa kama Yeye hata huko kwa BABA hajaenda,wewe unawezaje kutuaminisha hapa wale wema watakuwa paradiso hapohapo wanapokufa na waovu watakuwa kuzimu?

Hoja namba 3,haipaswi kuulizwa na mtu anayejiaminisha anajua maandiko kama wewe,bali mwanafunzi,hivyo nashangaa wewe kuuliza hilo swalii kwangu.

Naomba nihamie hoja namba 4 kama ulivyouliza,na kabla sijaanza kukujibu nikuulize swali,kipindi musa na eliya wanakuja na kuongea na masihi kuhusu habari za kufariki kwake,petro na yohana na yakono waliwatambua musa na eliya na hata petro aliwataja kwa majina yao bila kuwambiwa wala kutambulishwa na mtu,niambie aliwezaje kuwatambua wakati watu hao waliishi kizazi cha zamani sana zaidi ya miaka 2000 ilikuwa imepita na hajawahi kuwaona kabla?,

Sasa kabla sijakujibu zaidi,nacukua nafasi hii kuuthibitishia umma unaosoma uzi huu kuwa japo wewe mwenyewe unafanya kama vile unayajua maandiko,HUJUI LOLOTE SAWASAWA NA UANDIKACHO HAPA,HII NATHIBITISHA BAADA YA WEWE MWENYEWE KUULIZA SWALI NAMBA 4 HAPO JUU,AMBALO MTU MWENYE NURU SAWASAWA HAWEZI KUTUMIA MFANO HUO KUENDELEZA MAFUNDISHO YA UONGO JUU YA WAFU,hilo swali huwa linaulizwa na wote wasiojua maandiko huku wakilitumia fungu husika kupotosha watu wengine,naomba nikujibu vema ili nikutoe kwenye kutoamini na kuamini kinyume na kilichotakiwa kama ifuatavyo;

Kwanza tusome jinsi lilivyoandikwa kwenye vitabu vyetu: " Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi",katika fungu hili utaona wazi kuwa huyo mwizi na Yesu siku hiyo watakuwa peponi,hiyo ndio mana yake hasa kwa mujibu wa uandishi ulivyo.

Ila kwa msomaji wa biblia kwa maombi mengi ungekuwa umefunguliwa katika kifungo hiki kwa kujua kuwa Yesu na huyo mwizi wakifa hawatajua neno lolote bali kusubiri ufufuo,sasa kama wapo peponi na Mungu,maana naamini Mungu peponi yupo,kwanini waje kufufua mwili huu ulioharibika eti kwa kuunganisha roho na mwili,yaani mwili upo,then ili ufufuke ndio uungwe kweli na roho?,kinyume chake jibu swali roho ni nini?, piq kipindi anamfufua lazaro, aliita njoo huku nje,hakusema roho itoke peponi ije iungane na mwili ndio mwili tena utoke nje ya kaburi.

Katika fungu husika,msomaji anayejua maandiko angeweza kufunuliwa tu kuwa pale shida ni mahali alama ya koma ilipowekwa,na kitabu husika kina sehemu nyingi tu zilizowekwa muundo huo maana ni wanadamu huunganisha kitabu kile,sasa fungu lile yapaswa lisomeke hivi " Yesu akamwambia, Amin, nakuambia leo hivi,utakuwa pamoja nami peponi",yaani huyo mwizi alipaswa siku hiyo,saa hiyo (leo hivi) aamini kabisa kabla hajafa kuwa atakuwa na Yesu peponi,hii ndio maana ya fungu husika wala si kama utakavyo kuliweka.

Kwahiyo shida pale ni ile alama ya koma tu wala si maandishi katika fungu husika,kama ingekuwa hivyo basi Yesu angekuwa mwongo maana alisema akifa atakuwa katika moyo wa nchi yaani ardhi kwa siku 3,je peponi ni ardhini kwenye moyo wa nchi?,jibu ni dhahiri atakuwa kaburini,hadi hapa tu,elezea kwanini asingesema atakuwa peponi kwa siku 3 halafu atafufuka ila anasema atakuwa kwenye moyo wa nchi?
 
Mkuu naomba kuuliza, pale yesu aliposema "waacheni watoto wadogo waje kwangu ......,"' unaeza kuwa na uelewa juu ya kauli hii, yani kwanini hakusema '"waleteni watoto wadogo kwangu ...."? Kwako Mtumishi Rabbon
 
Wakuu mimi ndio kiranja mkuu huku kuzimu yote yaliyosemwa sio kweli. Narudia tena ni uwongo mtupu.

Kunyweni bia na pombe, sigara pori sijui shisha vuteni sana imbeni na fanyeni ibada kujifurahisha mwili. Huku hakuna mambo ya duniani kwa hiyo fanyeni mpaka mzeekee.

Huku ni kuzuri ila sio kama duniani. Kuna shida na karaha kuliko duniani. Sio sehemu ya kufikiria kuja ukiwa na nguvu. Ni bora ukae gerezani kuliko kuzimu huku haina vitu vya duniani.
 
mkuu hapa kuna masomo mengine, naomba uitazame koment yako hii kisha uyaandae, na kama yapo naomba un-tag huko tafadhl
 
Wakuu mimi ndio kiranja mkuu huku kuzimu yote yaliyosemwa sio kweli. Narudia tena ni uwongo mtupu.

Kunyweni bia sana imbeni na fanyeni ibada kujifurahisha mwili. Huku hakuna mambo ya duniani kwa hiyo fanyeni mpaka mzeekee.

Huku ni kuzuri ila sio kama duniani. Kuna shida na karaha kuliko duniani. Sio sehemu ya kufikiria kuja ukiwa na nguvu. Ni bora ukae gerezani kuliko kuzimu huku haina vitu vya duniani.
 
hapa nimekuelewa, ubarikiwe mkuu
 
umeeleza maana ya kaburi tu,tuelimishe maana ya kuzimu mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…