kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,261
- 1,785
Miaka kadhaa iliyopita nilimbambikiwa mtoto na dada mmoja maeneo ninayoishi japo ukweli hakufanana na mimi pamoja na kulalamika na kumwambia kuhusu tarehe zinavyokizana na ujauzito huo,kwa kuwa nilililewa na mila za kisukuma hasa babu zangu kuwa anawaambia baba zangu kuwa mtoto huwa hakataliwi na mimi nilikubali na kuanza kuhudumia matumizi pamoja na gharama mbalimbali hasa kipindi cha sikukuu ukizigatia mama mzazi wa huyo dada alikuwa anaogopwa sana kutokana na fani yake.
Ni rafiki yangu huyu alinisaidia kumnasa baba mwenye mtoto kwa kunipigia simu kuwa sasa baba mwenye mtoto amekuja kwenye nyumba aliyokuwa amepagisha huyo dada na wewe njoo ili tuelewe mbivu na mbichi.
Ukweli nilipofika pale kwanza nilikuta wanakunywa chai ila mwanamke akakimbilia chumbani na kumwacha mwanaume akiwa ameduwaa.
Nilimsalimia mwanaume mwezangu na kumuaga na tangia siku hiyo nikawa nimenawa na hadi leo ile gharama na usumbufu sijui mtoto amepatwa na hiki sijui kile hakuna tena na akahamia Sengerema toka maeneo ya Geita vijijini (Bukoli).
Kutokana na kushibana na rafiki yangu tulielewana kuwa endapo mmoja wetu akigundua viashiria vya hatari hasa kwa wanawake (girlfriend/ama mke) basi asisite kutoa taarifa hata kama mmoja wetu ataenda kumwambia mke/girlfriend wake potelea mbali.
Mwaka huu mwanzoni rafiki yangu alipata matatizo ya kikazi (private job) hivyo alikimbia na akabadili no za simu ila tukawa tunawasiliana kwa njia zingine hususani Facebook. Baada ya muda mfupi nilipata taarifa za wife wake kuwa anatembea na mtu flani ambaye mimi na rafiki yangu na watu kibao tunafahamu kuwa jamaa ni mwathirika (samahani kama takuwa nimekosea ama kuonekana nawanyanyapaa ndugu zangu).
Baadae nikaanza kufuatilia hadi nikajiridhisha pasipo shaka kuwa jamaa anammega shemeji yangu!
Jana nimemtumia sms fb nikimwambia nakumbuka Wema ulionifanyia kwa Consolatha kuhusu kumbambikiwa mimba,namimi takuhakikishia hauambukizwi maradhi yoyote mbele ya macho yangu na demu wako yeyote ninayemfahamu hivyo utakapoamua kurudi kabla hujafika kwako ama kwa demu wako yeyote fikia kwangu nikupe ushauri.
Japo ananisumbua sana kuwa nimwambie lkn nimemtuliza na baadae akanijibu kuwa; nafahamu unanipenda,unaniheshimu na tumetoka mbali hivyo tafika kwako kabla ya kufika kwenye familia yangu ama nyumba ndogo yangu.
Ndugu nimedhamiria akifika nimwambie wakapime na shemeji ila sitamwambia mwanaume anayemchukua maana tasababisha mauti ila sitakubari rafiki yangu aliyenisaidia mambo meeeengi kimaisha anase kizembe vile never.