Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,142
- 48,367
Februari 16,2026 Jopo la Majaji watatu Mheshimiwa Jaji Fahamu, J. Mheshimiwa Jaji Chuma, na Mheshimiwa Jaji Kamana, liliamua kuwa kifungu cha 194 cha sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act (CPA) ni kinyume cha Katiba kwa kuwa kinampa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai haki ya kipekee kuomba ulinzi wa shahidi bila kumpa mshtakiwa haki sawa, na pia kinaruhusu maombi ya kusikilizwa upande mmoja bila kuhakikisha haki ya kusikilizwa kwa upande mwingine.
Soma Mahakama Kuu: Kifungu kinachoruhusu kuficha mashahidi wa kesi ni batili na kinyume na Katiba
Sisi tusiojua Sheria tukashadadia kuwa kesho yake Lissu atapeleka hukumu ile mahakamani ili kwenye kesi yake kusiwepo na mashahidi wa uficho.
Kumbe Lissu angepeleka hukumu ile angefungua mlango kwa mawakili wa Serikali kukata rufani kupinga hukumu hiyo isitumike kwenye kesi ya Lissu.
Maana yake huu mwenendo wa Sasa wa hii kesi ungesimama kusubiri uamuzi juu ya rufani hiyo itakayokuwa imekatwa na Serikali.
Wakati rufani inasubiri kusikilizwa muda waliopangiwa kina Jaji Ndunguru ungekuwa unaisha hivyo baada ya maamuzi ya rufani kutoka ingebidi Lissu asubiri tena Jaji Mkuu awapangie tena hao majaji muda mwingine wa kusikiliza hiyo kesi ya Uhaini inayomkabili.
Kitendo cha Lissu kukaa kimya kimefanya kesi iendelee kusikilizwa huku mawakili wa Serikali wakitafuta mbinu mpya ya kuifanya hiyo kesi isikilizwe kwa muda mrefu.