Lipumba: Kuna matukio yanapangwa nje ya chama cha CUF ili kifutwe kwa vurugu

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,451
112,105
l-5.png


Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amesema ameandika barua maalumu kwa jukwaa la wahariri kuonesha kusikitishwa kwake na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano wa CUF na kusababisha waandishi kufanyiwa fujo.

Prof Lipumba ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ameyasema hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Azam Two na pamoja na mambo mengine amemtaka katibu mkuu wa CUF Maalim Seif wakae wazungumze ili wamalize tofauti zao na wakae wakijenge chama..

“Baada ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na ni jambo ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wa habari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu”.

“Vile vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya dola kwa hiyo vyombo vya dola vinalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa na Mkurugenzi wetu wa habari na uenezi”

“Mimi toka awali nimeeleza kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa mazungumzo tupate suluhu tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa nikimuita Maalim Seif aje ofisi bugurudi aweze kuzungumza afanye kazi zake kama katibu mkuu na mimi nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa na mgogoro huu na kuuruhusu kuendelea”

“Hivi sasa kupitia taarifa zetu za kiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna mbinu ya kutaka chama hiki kiweze kufutwa kwa hiyo kuna matukio yanapangwa nje ya chama ili paweze kutokea vurugu na zikishatokea waseme chama hiki hakifai kuendelea kuwa chama cha siasa na utakuta kuna vyama vingine vya siasa vinashabikia na kutoa wito ili chama hiki kiweze kufutwa” Prof. Lipumba

Chanzo: Malunde blog
 
Tunajua lipumba ndiyo yuko kwenye mkakati wa kuhahakikisha cuf inafutwa asiseme habari za uchunguzi.kumbe yeye ndiye alituma yule kijana akapige watu kwenye press Conference kama video zinavyoonyesha.ni aibu lipumba kutetea ujambazi ule anyway atleast we know anatumiwa
 
Lipumba amepewa kazi na ccm kuhakikisha analeta chokochoko ili CUF ifutwe na msajiri kwa lengo la kumkomoa Seif anayelalamika kuporwa ushindi wa urais na Shein.
 
Kama anania nzuri si achie hiyo nafasi kama alivyoamua kujiuzulu. Nia yake ovu ambayo anafanyia watanzania Mungu atampa hukumu kwani akumbuke wapinzani hapa nchini ni mgumu sana kwa hiyo wapo waliopoteza kazi zao maisha yao kisa ni kuwa upande wa upinzani kwa hiyo majibu yapo kumbuka historia hujirudia kwa uzuri au kwa ubayaa
 
Huyu jamaa alipata vp u-professor maana naona kama hajielewi. Ana laani tukio hilo at the same time asema kjana wao amekatwa kisigino means wale walio piga waandishi wa habari
 
kifutwe team SEIF watajiunga chadema, na team LIPUMBA mjiunge rasmi ccm
 
Kama sio yeye mwenyewe kuachia ngazi haya yote yangetokea wapi? Sasa anaonekana jinsi alivyo mamluki,mawazo binafsi ili abakie na heshima yake kama Dr Slaa ni bora akae china nakujipanga upya maana wananchi wanamuona kibaraka wa CCM.
 
Back
Top Bottom