Lionel Messi aweka rekodi mpya ya ufungaji Argentina ikitinga fainali Copa America

Buenos Aires

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,895
1,608
MFALME WA SOKA DUNIANI KUWAHI KUTOKEA LIONEL ANDRES MESSI AWEKA REKODI MPYA YA UFUNGAJI ARGENTINA IKITINGA FAINALI COPA AMERICA
Messi-record.jpg



Lionel Mesi sasa anaongoza orodha ya wafungaji katia taifa la Argentina baada ya kuopiga mkwaju wa free-kick uliozama moja kwa moja kambani wakati Argentina ikiiangamiza USA kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa nusu fainali kisha kufuzu fainali ya Copa America kwa mara ya pili mfululizo.

Star huyo wa Barcelona ameivunja rekodi ya Gabriel Batistuta ya magoli 54 baada ya kufunga bao lake la 55 kwa mkwaju wa adhabu ndongo umbali wa mita 25 kwenye ushindi wa Argentina wa magoli 4-0 dhidi ya United States.

Messi alisaidia kupatikana kwa bao la kwanza lililofungwa na Ezequiel Lavezzi, kisha akafunga bao la pili kabla ya striker wa Napoli Gonzalo Higuain kupachika bao jingine ma kuiweka mbele Argentika kwa bao 3-0.

Higuain alifunga bao jingine dakika ya 85 kumaliza mchezo huo uliowapeleka hatua ya fainali.

“Nimefurahi kuivunja rekodi ya Batistuta na nawashukuru wachezaji wenzangu ni rekodi yao pia,” amesema Messi ambaye Ijumaa atafikisha miaka 29.

Argentina itacheza fainali dhidi ya Colombia au mabingwa watetezi Chile ambao watacheza nusu fainali yao leo Jumatano June 22 huko Chicago.

Batistuta alitumia kambani bao 54 kwenye game 78 alizoichezea Argentina (lakini chama cha soka cha Argentina AFA hakihesabu magoli mawili ambayo alifunga dhidi ya Slovania wakati akiichezea timu ya vijana mwaka 1995) katika michuano ya kimataifa ambapo alianza kucheza tangu mwaka 1991 hadi 2002 na kufanikiwa kushinda mataji ya Copa Amerika mwaka 1991 na 1993 huku akifanikiwa kupiga hat-trick kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1994 na 1998.

Lakini Messi, 28, sasa alifanikiwa kuifikia rekodi hiyo alipofunga goli dakika ya 60 wakati Argentina ikiichapa Venezuela kwa bao 4-1 kwenye uwanja wa Gillette huko Marekani na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Copa America Centenario.

“Nimeifikia, bado sijaivunja. Lakini ninafurahi kufikia rekodi ya Bati, inamaana sana,” alisema Messi baada kumalizika kwa mchezo huo.

Kocha wa timu ya taifa ya Argentina Gerardo Martino alisema: Nadhani anafasi ya kuweka rekodi yake. Nitafurahi kama itatokea kwenye michuano ya Copa America.”

Star huyo wa Barcelona aliyefikisha magoli 55, anafukuzwa kwa karibu na wachezaji wenzake Sergio Aguero (33) na Gonzalo Higuain (28).

Magoli 55 aliyoifungia Argentina, 27 yametokana na mechi za kirafiki, 15 yakiwa ni magoli aliyofunga kwenye mechi za kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia, mabao nane kwenye michuano ya Copa Amerika na magoli mengine matano amepachika kwenye fainali za kombe la dunia.

Messi alitokea benchi na kufunga hat-trick Argentina iliposhinda kwa goli 5-0 dhidi ya Panama kwenye michuano ya Copa America, kwa ujumla amefunga magoli tisa akiingia kutoka benchi wakati magoli 46 ameyafunga akiwa ameanza kwenye kikosi cha kwanza.

Katika bao hizo 55, amefuka hat-trick nne, magoli 6 (yakiwa ni magoli mawili (double) kwenye mechi moja, huku magoli 31 akiwa amefunga mojamoja (single). Magoli 43 amefunga kawaida (open play) wakati magoli 11 yametokana na mikwaju ya penati.

Brazil na Paraguay ndiyo timu pinzani zaidi dhidi ya Messi, amefunga mara nne dhidi ya timu zote mbili, huku akifunga mara tatu dhidi ya timu nyingine saba.

Alicheza mechi yake ya kwanza kwenye timu ya taifa ya Argentina akiwa na miaka 18, mchezo wa kirafikia dhidi ya Hungary mwaka 2005 lakini akalimwa kadi nyekundu dakika mbili baada ya kuingia akitokea benchi na ilichukua mechi sita kufunga goli lake la kwanza kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Croatia mchezo uliokuwa wa kirafiki.

Goli lake la kwanza kwenye mechi ya mashindano lilikuwa dhidi ya Serbia and Montenegro wakati Argentina inashinda kwa magoli 6-0 kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2006 lakini ilibidi asubiri hadi February 2012 kufunga hat-trick yake ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Switzerland alipoisaidia Argentina kupata ushindi wa magoli 3-1.

Mesi alikuwa mchezaji wa pili wa Argentina kufikisha magoli 50 mwezi March mwaka huu alipofunga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Bolivia katika harakati za kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia
 
Hakuna ataekuja kuvunja records ya King,,labda baada ya miaka 2000 huo ndiyo ukweli
 
Huyu mfalme ni balaaaaa sanaaaa anatisha na kombe linaenda Albiceleste cheezea The king weeee utalala mlango wazi wanao mchukia hawajui maana ya mpira Respect, na siku ya final ataendelea kuongeza idadi ya magoli mpaka mupasuke na mpate Anxiety disorders
 
Messi mechi 112- magoli 55
Batistuta mechi 78- Magoli 54.
Halafu anasifia kuwa Messi ni zaidi!!? Huu ujuha uliopitiliza.
Watu wana mahaba hata shetani anawashangaa. Wamejitia kiwi machoni na akili zao nimenasa kwa messi wamekuwa kama wamelishwa limbwata. Ukiwaambia ukweli kama wanakuona wanaweza kukupiga hata na mawe.
 
Watu wana mahaba hata shetani anawashangaa. Wamejitia kiwi machoni na akili zao nimenasa kwa messi wamekuwa kama wamelishwa limbwata. Ukiwaambia ukweli kama wanakuona wanaweza kukupiga hata na mawe.
Yaani mi nawaona ni zaid ya mazuzu. Mashabiki uchwara tu kazi kujaza server kila kukicha humu za kumsifia, yaani nguvu wanayotumia kumpromo ni kubwa sana isiyo reflect kazi afanyayo.
 
Copa america kule siku hizi hakuna kitu ni sawa na Afrika tu.

Ndiyo maana timu kupigwa 5+ ni kawaida tu.

Mambo yote Ulaya bana, hao wengine wasindikizaji tu.

Ha ha ha! "Wachukiaji" hamuishiwi sababu. Kwani Ulaya watu hawafungwi 5? Ulaya watu wanafuata hela mpira uko Americana bhana!
 
Watu wana mahaba hata shetani anawashangaa. Wamejitia kiwi machoni na akili zao nimenasa kwa messi wamekuwa kama wamelishwa limbwata. Ukiwaambia ukweli kama wanakuona wanaweza kukupiga hata na mawe.

teh teh teh....ukimchukia messi dada ako atampenda na kibaya zaidi akikutana na timu yako anainyooosha kama kawaida.....!!! na ukileta record za yule unayeamini anajua mpira zinaangukia pua kwa huyu dogo...naamini unamdis ila unamkubali kiaina
 
Hakuna player yeyote tangu soka lianze kuchezwa hapa ulimwenguni aliyeweza kuiga hata robo tu ya wafalme hawa.. Diego Armando Maradona na Leonel Andres Messiah

Nimefarijika saana kuwaona hawa wachezaji raaaha tupu, wenye chuki na wawili hawa ajipige ukutani au ajinyonge kabisa
 
teh teh teh....ukimchukia messi dada ako atampenda na kibaya zaidi akikutana na timu yako anainyooosha kama kawaida.....!!! na ukileta record za yule unayeamini anajua mpira zinaangukia pua kwa huyu dogo...naamini unamdis ila unamkubali kiaina

Mkuu Trillionare huyo bwana asubiri tu j,tatu ya alfajiri pale marekani Albiceleste na Chile, final...ndio atamjua Mfalme ni nani hahaa..Vivaa Mfalme
 
Back
Top Bottom