Lini CHADEMA itatoa majina ya wabunge wa Afrika Mashariki?

OPENM

Member
May 27, 2014
7
10
Tangu uchaguzi wa tarehe 4/4 2014 kumalizika na kupatikana wabunge saba kama wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kumekuwa na sintofahamu nyingi juu ya wabunge wawili wanaopaswa kutoka CHADEMA.

Lawrence Masha na Ezekia Wenje kura zao hazikutosha ingawa wakati CHADEMA wanakilisha majina hayo walitaka yapite bila kupingwa kitendo ambacho ni kinyume na kanuni.Wabunge wa chama tawala walipinga suala hilo la kuletewa wabunge wawili kwani suala la jinsia halikuzingatiwa na zaidi majina hayo yalitoka katika mkoa mmoja wa Mwanza.

Baada ya uchaguzi huo kumalizika na matokeo kutangazwa mwenyekiti wa Chama hicho alisema mbele ya waandishi wa habari kuwa watarejesha majina hayo hayo yaliopigiwa kura nyingi za HAPANA japo hadi leo wamekaa kimya

Ni vema wakaweka mchakoto huu wazi kuliko kufanya siri wakati tayari baadhi ya wanachama wa CHADEMA wameshaanza kuyataja majina yaliyopendekezwa kuwa ni
  • REGINA LOWASSA, FREDERICK SUMAYE na PROF. MWESIGA BAREGU.
Ni vema tukakumbushana kuwa hili ni suala la kitaifa na si la kifamilia. Ni vema CHADEMA wakaonesha kukuwa kisiasa na kutolifanya suala hili la chumbani .

 
Back
Top Bottom