Ligi ya Zanzibar ikipata Wadhamini Safi itakua bora kuliko Ligi ya Bara.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Nimejaribu kufuatilia kombe la Mapinduzi linaloendelea nimegundua kwamba timu za Zanzibar ni bora sana hata kuliko za bara na ukiangalia ligi yao wala timu zenyewe hazina udhamini mkubwa kama ligi ya Bara.

Timu za Zanzibar zimekosa kitu kidogo tu anzia Ufundi mpaka Uzoefu ila ukiangalia mchezaji mmoja mmoja kuna vitu flani wanavyo vya kimpira ni kuongezewa maarifa kidogo tu kutoka kwa Makocha wazuri,Timu za Zanzibar zina aina flani za mpira wa kispaniola/Brazil wanaweka mpira chini sana na pasi fupi fupi wanavutia kuangalia kwa kweli tofauti na Bara wana mpira wa pasi ndefu na kukimbizana kwa sana(Man to man footbal/physic game).

Pia wachezaji wa Zanzibar wanajua kujitunza sana mfano ni hawa wachache wanaocheza Ligi ya bara,Canavaro,Selembe,Moris,Mwadini,kuna Abdi kasim yeye yupo Zanzibar.

Ushauri ni vizuri chama cha Soka Zanzibar kutafuta wadhamini wazuri ili ligi yao iwe bora turudi zama zile za timu kongwe kama Mlandege,Mlandizi,Kmkm,Miembeni(chelsea ya Zenji)...nk na Pia Azam angejitaidi kuwekeza kule hata ikiwezeka kuonyesha Mubashara ligi ya Zanzibar.

Aksanteni
 
wazamini wazuri ni makampuni ya bia kule hawawataki(maustadhi)
 
nadhani kuna udhamini mzuri pia zaidi ya makampuni ya bia kuna makampuni ya Simu,Maziwa,Benki mbalimbali,Vinywaji vingine baridi zaidi ya Bia
 
Kiukweli wako vizuri, kwanza marefa wao wanajua hawana kupendelea.Yani hawa maustadh wakipewa tu hata udhamini wa bil 8.Hakuna timu bara itakayo furukuta.
 
I have been said hawa jamaa wakipata ufadhili wapo sawa mnoo wana mpira flani wa kihispain na Kibrazil.
Sisi huku hata haijulikani tunacheza mpira gani

FT TANZANIA 1 ZANZIBAR 2
Hongereni vijana.
 
dah afadhal Leo watanganyika hamjaeka comments zenu za chuki na mumekiri kama hamna mlijualo
 
1. Tatizo la tanzania bara si mpira yaani soka per se, bali kuunda na ku-manage timu za taifa

2. Mpira unachezwa na watu 11. Nchi yenye watu kama milioni 1 hivi: zanzibar na watu milioni 45 tanzania bara, wanatakiwa kuweka kombinesheni nzuri ya wachezaji wenye nguvu na mafundi 11 tu kila mmoja. Sasa binadamu wengi wanafanana fanana ki maumbile na vipaji. Kati ya watu milioni moja unaweza kabisa kupata 11 ambao wanaweza kucheza popote duniani na dhidi ya yeyote yule.
3. Hivyo huwezi ku-assume kwamba kwa kuwa bara ni kubwa basi mtawafunga wale wenye population ndogo kwani wanaruhusiwa 11 tu.
4. The Cranes ya Uganda karibu robo tatu ya wachezaji wako pale kwa kama miaka 10 hivi wakati Kilimanjaro Stars imebadilika karibu mara 10 tangu enzi hizo na hatujaonyesha uwezo wa kuwafunga. Tatizo ni uongozi na utawala wa huu mchezo kwa timu za pamoja yaani taifa za Tanzania.

5. Zikiwa Club kama Azam, Simba, Yanga n.k. tangu makombe yote: Afrika Mashariki, mapinduzi, tusker timu za tanzania ndiyo mabingwa wa kihistoria, lakini si timu za taifa tatizo tumeshindwa formula ya kufanya viongozi na wachezaji wenye mapenzi tofauti kwa hivi vilabu wakafanya kitu cha maana pamoja wanaoneana aibu lakini wako pale kuangalia wachezaji wa timu wanazozipenda, utamaduni unaotakiwa kupigwa vita.
 
Nimejaribu kufuatilia kombe la Mapinduzi linaloendelea nimegundua kwamba timu za Zanzibar ni bora sana hata kuliko za bara na ukiangalia ligi yao wala timu zenyewe hazina udhamini mkubwa kama ligi ya Bara.

Timu za Zanzibar zimekosa kitu kidogo tu anzia Ufundi mpaka Uzoefu ila ukiangalia mchezaji mmoja mmoja kuna vitu flani wanavyo vya kimpira ni kuongezewa maarifa kidogo tu kutoka kwa Makocha wazuri,Timu za Zanzibar zina aina flani za mpira wa kispaniola/Brazil wanaweka mpira chini sana na pasi fupi fupi wanavutia kuangalia kwa kweli tofauti na Bara wana mpira wa pasi ndefu na kukimbizana kwa sana(Man to man footbal/physic game).

Pia wachezaji wa Zanzibar wanajua kujitunza sana mfano ni hawa wachache wanaocheza Ligi ya bara,Canavaro,Selembe,Moris,Mwadini,kuna Abdi kasim yeye yupo Zanzibar.

Ushauri ni vizuri chama cha Soka Zanzibar kutafuta wadhamini wazuri ili ligi yao iwe bora turudi zama zile za timu kongwe kama Mlandege,Mlandizi,Kmkm,Miembeni(chelsea ya Zenji)...nk na Pia Azam angejitaidi kuwekeza kule hata ikiwezeka kuonyesha Mubashara ligi ya Zanzibar.

Aksanteni

Uliona mbali sana.
 
Back
Top Bottom