Ligi ya nchi gani ndio bora sana duniani?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
wapenzi wa soka la nje,nchi gani kati ya hizi unadhani ina ligi yenye ushidani zaidi?
italia
uingereza
ujerumani
ufaransa
uhispania
uholanzi
 
Ok. Kwa ubora wa ligi ni Spain(La Liga). Kule kuna klabu bora kabisa duniani kwa sasa. Ila kwa ligi yenye ushindani na mashabiki wengi sana ni Uingereza(EPL)
 
Walio juu yangu wamechangia vzur na hawajabishiwa KIDUNIA LIGI BORA na NGUMU DUNIANI NI LA LIGA BBVA.
ligi bora na ngumu kivipi ili hali only madrid & barca wanawafunga wenzao mara goli 10, 7,6,5,4! ugumu upo wapi hapo??

EPL mara ya mwisho kusikia mtu kafungwa 10 ilikuwa lini??
 
hatutazami watu wanafungana vipi....kwa epl kikubwa ni kwamba timu hazitofautiani sana uwezo tofaut na spain...tazama zinavyofanya UEFA na eurpoa utafaham nn namaanisha ......ligi ya spain ina ubora ila epl ina mashabiki wengi
 
Ok. Kwa ubora wa ligi ni Spain(La Liga). Kule kuna klabu bora kabisa duniani kwa sasa. Ila kwa ligi yenye ushindani na mashabiki wengi sana ni Uingereza(EPL)
naweza kukubaliana nawewe kwa hilo lakini ukiangalia ligi ya spain wanaofanya vizuri ni timu mbili tu kwa mtazamo wangu hii haifanyi kuwa ligi yenye ushindani,ushindani huatikana kwa matokeo kuto tabirika
 
Soma vizuri mkuu. Nimesema EPL ya Uingereza ndo ligi yenye ushindani na mashabiki wengi ila HAINA ubora. Ukitaka kuamini kwamba haina ubora, we cheki UEFA Champions League. Wanalazwa kinoma
 
a

asante mkuu,nimekuelewa.
 
ligi bora na ngumu kivipi ili hali only madrid & barca wanawafunga wenzao mara goli 10, 7,6,5,4! ugumu upo wapi hapo??

EPL mara ya mwisho kusikia mtu kafungwa 10 ilikuwa lini??
Hakuna ligi ambayo hainivutii kama La Liga, ligi gana timu zinafungana kilofa vile, mara utasikia madrid kashinda 8, mara Barca kashinda 6-0.
Nitaendelea kuipenda ligi ya Epl daima, Atleast hata Bundes liga mzuri kuliko hiyo ligi wa kikuda.
 
Ushabiki utakuua wewe, hivi ukichukua hizo timu zinazo fungwa ukashindanisha na za epl, nn kinatokea?
 
Soma vizuri mkuu. Nimesema EPL ya Uingereza ndo ligi yenye ushindani na mashabiki wengi ila HAINA ubora. Ukitaka kuamini kwamba haina ubora, we cheki UEFA Champions League. Wanalazwa kinoma
Ubora je? Maana unasema umezungumzia ushindani?
 
Hakuna ligi ambayo hainivutii kama La Liga, ligi gana timu zinafungana kilofa vile, mara utasikia madrid kashinda 8, mara Barca kashinda 6-0.
Nitaendelea kuipenda ligi ya Epl daima, Atleast hata Bundes liga mzuri kuliko hiyo ligi wa kikuda.
Mkuu mkolaj, inashangaza sana hii ligi inayoitwa bora na ngumu-sijawahi ona barca/madrid anafungwa angalau 5 na timu yoyote za chini kinyume chake barca/madrid ndio kila siku wanapiga wenzao vpigo vinene vinene!

EPL juzi kati livapool amekula 6 kutoka stoke, aseno amekula 4 bila kutoka kwa soton!
 
Kiushindani hakuna kama epl ndo maana unakuta mpaka dakika ya mwisho ndo bingwa anapatikana na hata ukiangalia gaps kati ya timu na timu si kubwa.....yani epl hata kushuka daraja kuna upinzani ukizubaa kidogo ushapigwa gap umeshuka wewe daraja.....
Ubora kwa spain hakika wana timu bora ukizilinganisha na za uingereza kwa sasa....thn bundesliga inaweza kufatia.....angalia tu hata game ilopita europa totenham vs borussia both re 2nd in their league lkn hali ilikua mbaya kwa tot....
 
Mkuu mkolaj, inashangaza sana hii ligi inayoitwa bora na ngumu-sijawahi ona barca/madrid anafungwa angalau 5 na timu yoyote za chini kinyume chake barca/madrid ndio kila siku wanapiga wenzao vpigo vinene vinene!

EPL juzi kati livapool amekula 6 kutoka stoke, aseno amekula 4 bila kutoka kwa soton!

Unaelewa maana ya neno ushindani? Unaelewa ili ushindani uwepo vitu gani vinatakiwa?

Ili kuwe na ushindani ni lazima mlingane, either wote mjue au wote msijue. Ikitokea mmoja anajua mwingine hajui hakuwezi kuwa na ushindani.

Nakubali EPL ina ushindani na ushindani huo unatokana na kuwa timu zote zimelingana viwango. Viwango ni vidogo au vikubwa jibu tunalipata kwenye Champions League.

Arsenal mnayodai inatoka kwenye ligi ngumu/yenye ushindani akikutana na Barcelona mnaodai wanatoka kwenye ligi nyepesi matokeo yanajulikana hata kabla ya mechi.

Spain, German, na France timu inayojua inajua na asiyejua hajui. Haiwezekani bingwa mtetezi akutane na timu inayoshika mkia afungwe au watoke suluhu useme ni ushindani. Huo ni ujinga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom