Licha ya kuchemka katika Premier League, Manchester United yaifunika Real Madrid kwa utajiri

karanisi

Member
May 28, 2017
8
1
Licha ya kushika nafasi ya sita katika Premier League msimu wa 2016/17, Manchester United imetajwa kuwa ndiyo klabu yenye thamani kubwa zaidi Ulaya ikiifunika Real Madrid.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya KPMG imeonyesha kuwa Man United imekuwa na mafanikio makubwa kifedha zaidi ya Real Madrid na Barcelona licha ya kuwa United ina madeni makubwa.

Katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa ya kifedha, kuna klabu sita katika 10 bora. Siri kubwa ya United kuongezeka thamani ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki sehemu nyingi duniani na kutumia mitandao yao ya kijamii vizuri.

Utafiti huo ulifanyika kwa kutazama mafanikio ya kifedha katika msimu wa 2014/15 na 2015/16.

Bayern Munich inashika nafsi ya nne ikiguatiwa na Manchester City.

KLABU ZENYE THAMANI KUBWA ULAYA
1 Manchester United
2 Real Madrid
3 Barcelona
4 Bayern Munich
5 Manchester City
6 Arsenal
7 Chelsea
8 Liverpool
9 Juventus
10 Tottenham
11 PSG
12 Borussia Dortmund
13 Atlético Madrid
14 Schalke
15 Milan
16 Leicester
17 Everton
18 Roma
19 Inter
20 Napoli
21 Galatasaray
22 Fenerbahce
23 Benfica
24 Lyon
25 Athletic Bilbao
26 Ajax
27 Sevilla
28 Valencia
29 Lazio
30 Besiktas
31 PSV Eindhoven
32 Marseille

CHANZO: LICHA YA KUCHEMKA KATIKA PREMIER LEAGUE, MANCHESTER UNITED YAIFUNIKA REAL MADRID KWA UTAJIRI
 
Hiyo ni thamani, not tangible cash! Thamani inaporomoka muda wowote kama hisa tu..!
 
Arsenal bado wanatafuta pesa afu cha ajabu washazidiwa na man city
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom