LHRC wapinga IPTL kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme, wataka EWURA kuomba radhi watanzania

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
LHRC wamepinga kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited,
Wanasema kampuni hii inahusishwa na kashfa ya uchotaji wa mabilioni kupitia akaunti ya Escrow
na kamati ya bunge ya hesabu za serikali PAC mwaka 2014 ilitoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo juu ya umiliki wa mitambo ya IPTL ikiwemo TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya umiliki na uwepo wa rushwa na utendaji kazi wa IPTL na wabia wake, mapendekezo ambayo mpaka sasa hayajafanyiwa kazi na umma wa watanzani haujui kinachoendelea

Wameshangazwa na kitendo cha EWURA kuomba maoni kwa wadau huku mikataba ya serikali ikiwa ni siri hivyo wadau hawana sababu za kikataba za kutoa maoni
EWURA ilipaswa kujiridhisha kupitia juu ya mapendekezo ya bunge la tanzania kupitia ripoti ya kamati za hesabu za serikali juu ya utata wa umiliki wa IPTL na kashfa za rushwa badalaya kutaka maoni kutoka kwa wananchi ambao hawajui kilichopo kwenye mkataba

Wanatoa mapendekezo EWURA kusitisha zoezi la kukusanya maoni kutoka kwa wadau hadi serikali itakapofanyika kazi mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya bunge
Pia EWURA kujiridhisha uhalali wa umiliki, ushiriki wa IPTL katika akaunti ya Escrow na tuhuma za rushwa kwa wamiliki wake

EWURA kuomba radhi kwa watanzania na Bunge kwa kujaribu kuirudisha IPTL huku ikitambua miaka 3 iliyopita ilikumbwa na kashfa nzito ya rushwa
LHRC inawakumbusha watanzania wote kuungana kwa maslahi ya umma kukataa pendekezo hili

Pia serikali kutoa majibu na ufafanuzi juu ya utekelezaji wa maamuzi ya kamati ya bunge na kuacha mazingaumbwe kwa kuwashirikisha katika shughuli wasiokuwa na uelewa nazo bali wawe wazi ktikahatua zote za makubaliano na kuwakumbusha waandishi wa habari jinsi bunge lilivyosimama wakati wa kashfa hii
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,510
2,000
IPTL INA wenyewe,na wenyewe vigogo ccm.Leseni watapewa.Chezea capacity charge kila mwezi 3 bn
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,354
2,000
Ha ha ha,eti umiliki wa mitambo,,,
wabongo kwa kupenda vya bure hatujambo..

Yaani mitambo ya watu wameitolea jasho uipate kirejareja tu?

Escrow scandal yalikuwa majungu in reality
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
35,354
2,000
Ha ha ha,eti umiliki wa mitambo,,,
wabongo kwa kupenda vya bure hatujambo..

Yaani mitambo ya watu wameitolea jasho uipate kirejareja tu?

Escrow scandal yalikuwa majungu in reality
 

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,910
2,000
Namusubiri mzee wa misifa nione atachukua hatua gani hapa na kwa wazee wa mafurushi
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,477
2,000
IPTL ina wenyewe, ukiona kelele zinapigwa, matangazo kibao kutaka maoni, ni danganya toto. Na leseni itatolewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom