Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na Haki za binaadamu LHRC ina wajibu wa kutoa tamko la kukanusha juu ya upotoshwaji uliotolewa na Marekani juu ya kinachodaiwa kuwa nchi yetu inavunja haki za binadamu.
Nasema hivyo kwakuwa taasisi hiyo ipo nchini kwa kazi kubwa ya kusimamia na kulinda haki za binadamu na pia kuibua aina yoyote ya ukwiukwaji wa haki za binadamu.
Ripoti ya kila mwaka inayotolewa na taasisi hiyo haionyeshi kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.
Kilichofanywa na Marekani ni upotoshaji wa maksudi wenye nia ya kuchafua heshima ya nchi yetu.